ICC

15 Novemba 2019

Hii leo ni mada kwa kina tukibisha hodi Bukoba mkoani Kagera nchini Tanzania ambako Nicolaus Ngaiza wa radio washirika Kasibante FM amezungumza na mgonjwa wa kisukari akielezea madhila anayopitia kisha neno la wiki RIKISHA.

Sauti -
9'55"

08 jULAI 2019

Jaridani leo Jumatatu ya Julai 8, 2019 na Flora Nudhc pata habari kuhusu:

Sauti -
12'58"

12 Aprili 2019

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet, leo ameukumbusha uongozi wa Sudan kuhusu wajibu wake kimataifa wa kuhakikisha unalinda haki za binadamu kwa watu wote na kujizuia na machafuko.

Sauti -
9'57"

Majaji wa ICC watupilia mbali ombi la Bensouda la kuchunguza Afghanistan

Majaji wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC hii leo kwa kauli moja wametupilia mbali ombi la mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo Fatou Bensouda ya kutaka kufanya uchunguzi dhidi ya kile kinachodaiwa kuwa ni  vitendo vya uhalifu wa kivita na kibinadamu vilivyofanyika nchini Afghanistan.

Kufutiwa viza ya Marekani hakumzuii Bensouda kuendelea na majukumu yake- ICC

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC, imethibitisha kuwa serikali ya Marekani imefuta kibali cha kuingia nchini humo cha mwendesha mashtaka mkuu huyo Fatou Bensouda.

Hatimaye Ngaïssona wa CAR akabidhiwa ICC

Hii leo, Patrice-Edouard Ngaïssona ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita na dhidi ya binadamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, amekabidhiwa kwa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC huko The Hague, Uholanzi.

Mwendesha mashtaka ICC ashindwa kuthibitisha makosa dhidi ya Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire!

Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC leo imemwachia huru rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo na aliyekuwa mkuu wa tawi la 

Sauti -
1'49"

15 Januari 2019

ICC yawaachia huru Gbagbo na  Blé Goudé Wakimbizi wa Burundi waendelea kurejea nyumbani. Nilivutiwa kuwa daktari kw

Sauti -
12'25"

ICC yawaachia huru Gbagbo na Blé Goudé

Mahakama ya kimataifa ya makossa ya jinai, ICC leo imemwachia huru rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo na aliyekuwa mkuu wa vijana Charles Blé Goudé baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha pasipo shaka mashtaka yote dhidi yao. Arnold Kayanda na taarifa zaidi.

DRC Jiepusheni na uhalifu wakati wa uchaguzi la sivyo mtawajibishwa- ICC

Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC tarehe 23 mwezi huu, mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC imeonya kuwa yeyote yule nchini humo ambaye atachochea, ama atashiriki katika fujo kwa kuamuru, kutaka ama kuhimiza au kuchangia kwa njia yoyote ile au kutenda makosa yaliyo chini ya mamlaka ya ICC atashtakiwa na kufikishwa mbele ya mahakama.