Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa majanga ya magonjwa waeleza wasiwasi wao juu ya kuenea kwa mafua ya ndege kwa binadamu

Wataalamu wa majanga ya magonjwa waeleza wasiwasi wao juu ya kuenea kwa mafua ya ndege kwa binadamu.
© Unsplash/Obie Fernandez
Wataalamu wa majanga ya magonjwa waeleza wasiwasi wao juu ya kuenea kwa mafua ya ndege kwa binadamu.

Wataalamu wa majanga ya magonjwa waeleza wasiwasi wao juu ya kuenea kwa mafua ya ndege kwa binadamu

Afya

Madaktari wakuu wa Umoja wa Mataifa hii leo wamesema kuwa kuenea ulimwenguni kwa maambukizi ya ugonjwa wa  "mafua ya ndege" kwa mamalia wakiwemo binadamu ni suala muhimu la afya ya umma ambapo wametangaza hatua mpya za kuchukua kukabiliana na magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya hewa.

Dkt. Jeremy Farrar, Mwanasayansi Mkuu katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO), amesema kuwa virusi vinavyoeneza ugonjwa wa mafua ya ndege –H5N1 - vimekuwa na kiwango cha "juu sana" cha vifo kati ya mamia ya watu wanaojulikana kuwa wameambukizwa. mpaka sasa.

Hadi sasa, hakuna maambukizi ya H5N1 kutoka kwa binadamu Kwenda kwa binadamu ambayo yamerekodiwa.

"H5M1 ni (maambukizi) ya mafua, ambayo yalianzia kwa kuku na bata na yameenea kwa kiwango cha juu katika kipindi cha mwaka mmoja au miwili iliyopita na kuwa janga la zoonotic - wanyama - duniani," amesema Dkt Farrar.

"Wasiwasi mkubwa, bila shaka, ni kwamba katika kufanya hivyo na kuwaambukiza bata na kuku - lakini sasa wanazidi kuwa mamalia - kwamba virusi hivi sasa vinabadilika na kukuza uwezo wa kuambukiza wanadamu. Na kisha kwa umakini, vina uwezo wa kufanya maambukizi ya mwanadamu kwenda kwa mwanadamu.

Siri ya ng'ombe

Akizungumzia mlipuko unaoendelea wa virusi vya H5N1 miongoni mwa ng'ombe wa maziwa nchini Marekani, afisa mkuu wa WHO alihimiza ufuatiliaji wa karibu zaidi na uchunguzi wa mamlaka ya afya ya umma, "kwa sababu inaweza kubadilika na kuenea kwa njia tofauti".

Aliongeza: “Je, miundo ya kukamua ng’ombe hutengeneza erosoli? Je, ni mazingira wanayoishi? Je, ni mfumo wa usafiri unaoeneza haya kote nchini? Hili ni jambo la kutia wasiwasi sana na nadhani inabidi … kuhakikisha kwamba kama H5N1 ingewapata binadamu wenye maambukizi kutoka kwa binadamu hadi kwa binadamu, kwamba tungekuwa katika nafasi ya kujibu mara moja kwa kupata chanjo, matibabu na uchunguzi kwa usawa.”

Sawa na janga linalofuata

Taarifa hii inakuwa wakati WHO ilipotangaza kuboresha lugha ya kuelezea vimelea vya magonjwa vinayosambazwa kwa njia ya hewa, katika nia ya kuongeza ushirikiano wa kimataifa katika tukio la janga jipya - na linalotarajiwa - la kimataifa.

Hapo awali mpango huo ulichochewa na dharura ya COVID-19 na kutambuliwa kwamba kulikuwa na ukosefu wa masharti yaliyokubaliwa kati ya madaktari na wanasayansi kuelezea jinsi vizuri vya corona vilivyopitishwa, hali ambayo iliongeza changamoto ya kukabiliana na janga hilo, Dk Farrar alielezea.

Wito kimataifa

Ili kukabiliana na hali hii, WHO iliongoza mashauriano na mashirika manne makubwa ya afya ya umma kutoka Afrika, China, Ulaya na Marekani, kabla ya kutangaza makubaliano kuhusu idadi ya masharti mapya yaliyokubaliwa. Hizi ni pamoja na "chembe za kupumua zinazoambukiza" au "IRPs", ambazo zinapaswa kutumika badala ya "erosoli" na "matone", ili kuepuka mkanganyiko wowote kuhusu ukubwa wa chembe zinazohusika.

Zaidi ya istilahi mpya, mpango huo unasisitiza dhamira ya jumuiya ya kimataifa kukabiliana na "milipuko migumu zaidi na ya mara kwa mara", Dk Farrar aliwaambia waandishi wa habari huko Geneva Uswisi.

"Ni hatua muhimu sana ya kwanza. Lakini ijayo, tunahitaji kuweka taaluma, wataalam pamoja.

"Tunatumia istilahi sawa, lugha sawa, na sasa tunahitaji kufanya sayansi ambayo inatoa ushahidi juu ya kifua kikuu, juu ya COVID na vimelea vingine vya kupumua, ili tujue jinsi ya kudhibiti maambukizo hayo bora kuliko tulivyofanya huko nyuma."

Kuhusu hatari inayoweza kutokea ya HN51 kwa afya ya umma, Mwanasayansi Mkuu wa WHO alionya kwamba uundaji wa chanjo haukuwa "pale tunapohitaji kuwa". Wala haikuwa hivyo kwamba ofisi za kanda na ofisi za nchi na mamlaka za afya ya umma duniani kote zina uwezo wa kutambua H5N1, alisisitiza.