Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Paulina Ngurumwa: Mwanamke anahusika katika uzalishaji uchumi ambao hanufaiki nao

Paulina Ngurumwa kutoka KINNAPA Development Programme, shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa na wanajamii ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, kaskazini mwa Tanzania.
UN News

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kinara wa elimu nchini Tanzania Paulina Ngurumwa anasema bado kazi ipo kupigania haki za mwanamke kwa hiyo harakati hizo hazitakiwi kupoa. Paulina Ngurumwa ni mwanaharakati wa haki za kijamii kupitia shirika la KINNAPA Development Programme. 

KINNAPA Development Programme ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa na wanajamii ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, kaskazini mwa Tanzania likiwa ni chombo cha kutatua matatizo yao hasa ya ardhi. Shirika hili lilianzishwa mwaka 1992 na kwa miaka hiyo yote linajivunia kuendelea kufanikisha malengo yake na sasa hata limepanua mawanda ya huduma zake kama anavyoeleza mmoja wa viongozi Paulina Nguruma, katika mahojiano aliyoyafanya na Anold Kayanda wa Idhaa hii hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.