Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya ya kinywa ni suala linaloendelea kupuuzwa licha ya madhara yake: WHO

Kinywa na meno yenye afya njema ni sehemu muhimu ya afya ya mtoto.
© WHO
Kinywa na meno yenye afya njema ni sehemu muhimu ya afya ya mtoto.

Afya ya kinywa ni suala linaloendelea kupuuzwa licha ya madhara yake: WHO

Afya

Magonjwa ya kinywa, ingawa kwa kiasi kikubwa yanazuilika, husababisha mzigo mkubwa wa kiafya kwa nchi nyingi na huathiri watu katika maisha yao yote, na kusababisha maumivu, usumbufu, kulemaa na hata kifo kwa mujibu wa sjirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO huku ikikadiriwa kuwa magonjwa ya kinywa huathiri takriban watu bilioni 3.5 duniani kote.

Katika siku ya kuadhimisha afya ya kinywa hii leo WHO imesema kwamba matitizo ya kuuza kwa meno yasiyotibiwa na hasa katika meno ya kudumu ni moja ya magonjwa ya afya yaliyoenea zaidi. 

Limeongeza kuwa matibabu ya afya ya kinywa ni ghali na kwa kawaida si sehemu ya huduma ya afya kwa wote (UHC) hali inayochochea changamoto hiyo kuendelea.

Afrika ni changamoto kubwa

Kwa mujibu wa shirika hilo magonjwa ya kinywa, kama vile kuoza kwa meno, magonjwa ya fizi, na upotevu wa meno, bado yanaenea katika Kanda ya Afrika ya WHO, na kuathiri karibu asilimia 44 ya watu. 

Akizungumzia changamoto hiyo mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshidiso Moeti amesema  “Licha ya hatua za kiubunifu za timu yetu ya kikanda, eneo letu limekuwa na ongezeko kubwa zaidi la visa vya magonjwa makubwa ya kinywa katika miaka 30 iliyopita kati ya kanda sita za WHO. Habari njema, hata hivyo, ni kwamba magonjwa mengi ya kinywa yanaweza kuzuilika kupitia kudhibiti mambo hatarishi ya kawaida, kama vile kuepuka utumiaji wa tumbaku na pombe, kula chakula bora kisicho na sukari iliyoongezwa, na kuswaki meno kwa dawa ya meno yenye fluoride mara mbili kwa siku.”

Ameongeza kuwa afya ya kinywa inasalia kuwa sehemu iliyopuuzwa ya huduma ya afya inayomhusu mtu na ustawi wake.

Kupuuzwa kwa afya ya kinywa katika Kanda ya Afrika ya WHO amesema ni dhahiri ukiangalia katika kiwango cha chini ya uwekezaji. 

“Kwa mfano, nusu ya nchi katika Kanda ya Afrika ya WHO hazina sera za afya ya kinywa. Mwaka wa 2019, zaidi ya asilimia 70 ya nchi za eneo hilo zilitumia chini ya dola moja ya Kimarekani kwa kila mtu kwa mwaka kwa gharama za matibabu ya huduma ya afya ya kinywa.”

Ameendelea kusema kuwa zaidi ya hayo, kuna upungufu wa kudumu wa afya ya kinywa katika kanda, kwa mfano, kuna na madaktari wa meno 0.33 tu kwa kila watu 10,000, ambayo ni sehemu ya kumi tu ya wastani wa kimataifa.

WHO inaendelea kuwekeza Katia afya ya kinywa

Dkt. Moeti amesema timu za kikanda zinaendelea kuwekeza katika kuimarisha uwezo wa nchi katika kukuza afya ya kinywa, kuzuia magonjwa ya kinywa na timu yetu inaunganisha hili kama sehemu ya kuzuia na kuyadhibiti magonjwa yasiyoambukiza katika mifumo ya kitaifa ya utoaji wa huduma za afya kuelekea huduma ya afya kwa wote.

Dkt. Moeti ameongeza kuwa “Tunazipongeza Burkina Faso, Lesotho, Mali, Nigeria, na Sierra Leone kwa kubuni na kutekeleza sera za kitaifa za afya ya kinywa mwaka wa 2023. Tunatambua uongozi thabiti wa Nigeria na nchi nyingine 14 za Afrika miongoni mwa nchi 32 duniani ambazo zilisababisha kutambua rasmi noma kama mojawapo ya magonjwa ya kitropiki yaliyopuuzwa mwezi Desemba.