Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunatamani  sheria ya elimu Tanzania itambue wasichana kuendelea na masomo baada ya ujauzito

Nasra Kibukila kutoka shirika la TEN/MET nchini Tanzania.
UN News/Anold Kayanda
Nasra Kibukila kutoka shirika la TEN/MET nchini Tanzania.

Tunatamani  sheria ya elimu Tanzania itambue wasichana kuendelea na masomo baada ya ujauzito

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Nasra Kibukila akiwakilisha Shirika la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) katika Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani ulioanza Machi 11 hadi Machi 22, 2024 jijini New York, Marekani amezungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na kueleza wanayoyatekeleza nchini Tanzania ili kuhakikisha elimu bora hususani kwa wasichana.

 

Shirika la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MeT) ni moja ya mashirika ambayo kupitia ushirikianno na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) na kwa ufadhili wa Malala Fund na wadau wengine yanayohamasisha Lengo namba 4 la Maendeleo Endelevu kuhusu Elimu Bora na lengo namba 5 linalohimiza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana kwani yanaweza kufanikisha kufikiwa kwa malengo mengine ya maendeleo endelevu kama vile afya bora na ustawi na kutotomeza umaskini.