Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

GAZA: Sitisho la mapigano ni muhimu kuelekea mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani

Raia huko Ukanda wa Gaza wakiwa wamepanga foleni wakisubiri chakula
© UNRWA

Haki za binadamu

Mashambulizi yoyote ya jeshi la Israel dhidi ya eneo la Rafah lenye watu zaidi ya milioni 1.5 waliosaka hifadhi kufuatia ukimbizi utokanao na mapigano kwenye eneo hilo la Gaza, kutaongeza zaidi hatari ya uhalifu wa kivita, amesema Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Volker Türk hii leo.

Jeremy Laurence, ambaye ni msemaji wa Bwana Türk amewaeleza waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi hii leo kuwa hali ya sasa ambayo tayari ni janga inaweza kutumbukiza watu kwenye korongo zaidi  siku zijazo iwapo jeshi la Israel litaongeza zaidi operesheni zake kwenye mji huo wa kusini, kufuati tishio lao kuwa watashambulia iwapo Hamas hawatasalimisha mateka waliosalia kabla ya kuanza kwa kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Waislamu duniani kote wanaanza mwishoni mwa wiki hii kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, “kipindi ambacho kinamaanisha kuheshimu amani na stahmala,” amesema Bwana Laurence.

Raia wa Gaza ambao hawana pa kwenda hivi sasa wanaishi kwenye mazingira dhalili huko Rafah. “Mashambulizi yoyote ya ardhini huko Rafah yanaweza kusababisha vifo vya watu wengi na yataongeza hatari ya kiwango kikubwa cha uhalifu.”

Amesema hilo halipaswi kuachiliwa kutokea. “Tunahofia pia vikwazo zaidi vya Israel dhidi ya wapalestina kuingia Yerusalem Mashariki na msikiti wa Al Aqsa wakati wa mfungo wa Ramadhani kunaweza kuchochea mvutano zaidi.”

Mkuu huyo wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa amerejelea wito wake ya kwamba “lazima mzozo huu uishe mara moja na mauaji na uharibifu lazima vikome.”

Achia huru mateka bila masharti

Mateka waliotekwa nyara na Hamas na wanamgambo wengine wa kipalestina tarehe 7 mwezi Oktoba mwaka jana wamepitia siku 150 za machungu, amesema Bwana Türk, huku akitoa wito wa mateka hao kuachiliwa huru bila masharti yoyote na warejee makwao.

Na katika mashambulizi yake yanayoendelea, Israel kama nchi inayokalia kimabavu Palestina, “lazima izingatie wajibu wake kwa mujibu wa sheria ya kibinadamu ya kimataifa wa kupatia chakula na huduma za matibabu raia wa Gaza wanaohaha kukimu mahitaji yao, na iwapo haiwezi kufanya hivyo, ihakikishe raia ho wana fursa ya kufikia huduma hizo za kibinadamu.”

Halikadhalika, njia za kupita mpakani na kwingineko lazima zifunguliwe bila vikwazo na hatua zichukuliwe kuhakikisha misafara ya misaada inafikia raia kokote waliko.

Upanuzi wa makazi ya walowezi unakiuka sheria ya kimataifa

Bwana Türk pia hii leo amelaani uamuzi wa hivi karibuni zaidi wa Israel wa kujenga nyumba nyingine zaidi 3,476 kwenye eneo linalokaliwa la Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan, akisema “kasi hii ya kupanua makazi inaongeza mwenendo uliodumu wa ukandamizi, ghasia na ubaguzi dhidi ya wapalestina.”

“Ripoti za wiki hii kwamba Israel inapanga kujenga makazi zaidi 3,476 ya walowezi huko Maale Adumim, Efrat na Kedar ni pigo kwa sheria ya kimataifa,” ameongeza.

Katika ripoti yake kwa Baraza la Haki za Binadamu   Bwana Türk amesema kuanzishwa na kupanua makazi hayo kunaonesha nia ya Israel ya kuhamishia raia wake kwenye maeneo inayokalia, kitendo ambacho ni uhalifu wa kivita kwa mujibu wa sheria ya kimataifa.

Ripoti hiyo inayohusisha kipindi cha kuanzia tarehe 1 Novemba 2022 hadi Oktoba 31 mwaka 2023 inaainisha kuwa takribani nyumba 24,300 zilizoko eneo la makazi ya walowezi huko Ukingo wa Magharibi ziliendelezwa, ikiwa ni idadi kubwa tangu mwaka 2017. Hii inajumuisha takribani nyumba 9,670 huko Yerusalem Mashariki.

Ripoti imebaini kuwa sera za serikali ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu zinalandana kwa kiasi kikubwa na vuguvugu la walowezi wa Israel la kupanua udhibiti wao Ukingo wa Magharibi, ikiwemo Yerusalem Mashariki, na hatimaye kujumuisha eneo hili linalokaliwa kwenye taifa la Israel.