Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiwango cha vifo vya watoto Gaza bado cha juu-UNRWA

UNICEF yapeleka msaada wavifaa vya  kimatibabu kwa watu 70,000 katika Ukanda wa Gaza
UNICEF SoP
UNICEF yapeleka msaada wavifaa vya kimatibabu kwa watu 70,000 katika Ukanda wa Gaza

Kiwango cha vifo vya watoto Gaza bado cha juu-UNRWA

Haki za binadamu

Idadi ya watoto wachanga waliofariki dunia licha ya kupungua muongo uliopita kwingineko, bado ni kubwa kwenye eneo la Gaza.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti  mpya   ya shirika la Umoja wa Mataifa  linalohusika na kutoa msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA iliyochapishwa leo katika jarida la Plos One.

Ripoti hiyo Mkwamo wa kupungua kwa vifo  vya watoto wachanga  kwa wakimbizi wa kipalestina walioko Ukanda wa Gaza  tangu 2006,   inasema kuwa  kwa kila watoto 1000 wanaozaliwa wakiwa wazima wanaofariki dunia ni 22.7.

Kiwango hicho hakitofautiani sana na vifo vya watoto 22.4 katika kila watoto 1000, waliozaliwa  mwaka wa 2015 au kiwango cha watoto 20.2 kati ya watoto 1000 waliozaliwa   mwaka 2006.

 

Jamie McGoldrick (wa pili kushoto) ambaye ni Naibu Mratibu Maalum wa UN kwenye mchakato wa amani Mashariki ya Kati, akitembelea mgonjwa kwenye hospitali ya Al Quds huko Gaza
OCHA/Mustafa El Halabi
Jamie McGoldrick (wa pili kushoto) ambaye ni Naibu Mratibu Maalum wa UN kwenye mchakato wa amani Mashariki ya Kati, akitembelea mgonjwa kwenye hospitali ya Al Quds huko Gaza

Mkurugenzi wa idara ya afya ya UNRWA, Dkt. Akihiro Seita, amesema kuwa matokeo haya ni alama ya onyo  na mwelekeo wa hatari siyo tu kwa afya kwa watoto bali pia kwa afya ya wakimbizi wote wakipalestina walioko Gaza.

Ameendelea kuwa hili ni onyo kwa hali za kijamii na kiuchumi kwa eneo la Gaza kwani wakimbizi wa Palestina ni zaidi ya asilimia 70 ya idadi ya watu wote wa Gaza. “Vifo vya watoto ni kipimo cha afya ya watu wote,” amesema Dkt. Seita.

Vifo vya watoto ni kipimo cha afya ya watu wote

Afisa huyo wa UNRWA pia amesema kuwa matokeo ya uchunguzi huo yanahitaji kushughulikiwa kwani lengo lao ni kupunguza vifo vya watoto wanaozaliwa na vilevile  kuzuia vifo vya watoto vinaovyoweza kuepushwa.

UNRWA inasema Gaza ilishindwa   kutimiza lengo namba 4 la malengo ya maendeleo ya mileniala kupunguza kwa theluthi mbili vifo vya watoto wenye umri uli ochini ya miaka mitano.

Hali ya kijamii na kiuchumi huko Gaza zilibadilika katika katika muongo uliopita, kufuatia migogoro mbalimbali na mzingiro uliowekwa.

Mzingiro huo umeathiri sekta ya afya katika eneo la Gaza ambapo hospitali hazina miundo mbinu muhimu kama vile dawa na vifaa vingi vinginevyo vya matumizi muhimu.