Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Karne katika kuhabarisha, kuburudisha na kuelimisha - Siku ya Redio 2024

Redio ya zamani kutoka Makumbusho ya Mkusanyiko wa Scarborough Fair, iliyoko Scarborough, North Yorkshire, Uingereza.
Unsplash/Mike Hindle
Redio ya zamani kutoka Makumbusho ya Mkusanyiko wa Scarborough Fair, iliyoko Scarborough, North Yorkshire, Uingereza.

Karne katika kuhabarisha, kuburudisha na kuelimisha - Siku ya Redio 2024

Utamaduni na Elimu

Leo ulimwengu unaadhimisha Siku ya kimataifa ya redio duniani, dhima ya mwaka huu ikiwa 'Karne katika kuhabarisha, kuburudisha na kuelimisha'. Mwaka 2011 nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni (UNESCO) walipendekeza uwepo wa maadhimisho haya na mwaka mmoja baadaye Baraza kuu la Umoja wa Mataifa likapitisha likaidhinisha.

Radio inasalia kuwa chombo kinachotumiwa zaidi na chenye uwezo wa kipekee wa kuifikia hadhira kubwa zaidi kwa wakati mmoja kupitia aina tofauti ya maudhui. Chombo hicho kinasalia kuwa chombo salama na cha kuaminika wakati wa majanga ya asili yanayosababishwa na binadamu kama Mabadiliko tabianchi, Dhoruba, matetemeko ya ardhi, mafuriko, ajali na hata vita. 

Baadhi ya wananchi wa Afrika Mashariki wanaeleza umuhimu wa chombo hiki kinachoendelea kuuhudumia ulimwengu kwa zaidi ya miaka 100 sasa. 

Ni majira ya saa moja na dakika 26 za usiku kwa saa za afrika ya mashariki, licha ya kwamba umeme hauwaki na kawaida wakazi wa mkoa wa Geita ulioko kaskazini magaharibi mwa Tanzania, raia wa eneo hili hupenda kusikiliza radio zinazounganishwa na moja kwa moja na na umeme

Mmoja wao ni Sudy Shaban Maganga mwenye umri wa miaka 65.

Vijana wafuatilia vipindindi vya redio vya kukabiliana na changamoto katika jamii nchini Kenya. Vijana wahamasishwa kupitia programu za redio.
UNICEF
Vijana wafuatilia vipindindi vya redio vya kukabiliana na changamoto katika jamii nchini Kenya. Vijana wahamasishwa kupitia programu za redio.

Siku hii hutoa fursa kutambua mchango wa Radio, kama chombo cha kuaminika na chenye gharama nafuu zaidi duniani ambacho hutumika kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha jamii.

Watangazaji wa radio ambao ndiyo wazalishaji wapelekaji wa maudhui yaliyokwisha kuchakatwa na wahariri, anasema bado chombo hicho kina nafasi kubwa katika katika jamii.

Edgar Rwenduru, ni mtangazaji kutoka storm fm ya mkoani Geita.

Licha ya teknojolojia ya dijitali kuonesha kuwa tishio dhidi ya redio na kuonekana kuwa vijana wanaweza kuhamia kwenye vyanzo vingine vya habari, lakini bado kijana Kevin Keitany, wa Kajiado nchini Kenya alikuwa na sababu nzito za kuanzisha kituo cha redio Kajiado.

Na je Radio ambayo ni muelimishaji mkubwa inachangia vipi kuleta amani katika Jamii? Rose Haji kutoka nchini Tanzania Mwanahabari na mtangazaji nguli, anaeleza.

Kwa miongo miwili sasa, radio imekuwa ikikutana na mchuano/ mnyukano mkali kutoka kwenye majukwaa ya habari kama vile facebook, X, na Instagram ambapo watu hupata habari kwa uharaka zaidi ukilinganisha na miongo minne iliyopita, ambapo walisubiria muda fulani kusikiliza Muhktasari  wa habari au taarifa ya habari ama kupitia vipindi ambavyo vinatoa taarifa kila wakati ili kusikia nini kinaendelea duniani, lakini kwa sasa mambo yamebadilika.

Lakini swali la kujiuliza ni je radio itaendelea kuwa chombo cha kuaminika kwa zaidi ya muongo mmoja au karne mbili zijayo?