Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtu 1 kati ya 5 wanaoishi kwenye maeneo yenye mizozo ana matatizo ya akili:WHO/Lancet

Mgonjwa wa matatizo ya akili.
World Bank/Dominic Chavez
Mgonjwa wa matatizo ya akili.

Mtu 1 kati ya 5 wanaoishi kwenye maeneo yenye mizozo ana matatizo ya akili:WHO/Lancet

Afya

Makadirio mapya yaliyotolewa leo na shirika la afya ulimwenguni WHO yanaelezea haja ya kuongeza uwekezaji katika kuelendeza huduma za afya ya akili kwenye maeneo yaliyoathirika na vita.

Kwa mujibu wa tathimini iliyofanyika kutokana na tafiti 129 na kuchapishwa leo na jarida la afya la Uingereza Lancet, mtu 1 kati ya 5 au asilimia 22 ya watu wanaoishi katika maeneo yaliyoghubikwa na vita wana matatizo ya  msongo wa mawazo, wasiwasi, sonona ya kila wakati (PTSD), mtu kuwa na tabia mbili tofauti kuhusiana na suala moja na wazimu na huku asilimia 9 ya watu wote katika maeneo hayo ya migogoro wakielezwa kuwa na matatizo ya afya ya akili ya kiwango kidogo au cha wastani. 

Na idadi hiyo kimataifa ni kubwa kuliko ilivyokadiriwa hapo awali makadirio yaliyosema kuwa ni mtu 1 kati ya 14 katika maeneo yenye vita ndio ana matatizo ya afya ya akili.

Kwa mujibu wa WHO msongo wa mawazo na sonona vinaonekana kuongezeka kutokana na umri katika mazingira ya vita na msongo wa mawazo unawaathiri zaidi wanawake kuliko wanaume.

Hali halisi.

Matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba tathmini zilizopita zilikadiria vibaya mzigo wa matatizo ya afya ya akili katika maeneo yenye mizozo huku kiwango cha juu kikiwa asilimia 5 katika utafiti wa hivi sasa ikilinganishwa na asilimia 3-4 katika makadirio yaliyofanywa mwaka 2005, na kwa waathirika wa kiwango cha chini au cha wastani utafiti mpya unaonyesha kwamba ni asilimia 17 ikilinganishwa na asilimia 15-20 katika kipindic ha miezi 12 .

Makadirio haya mapya yametumia tafiri 129 zilizofanywa katika nchi 39 na kuchapishwa kati yam waka 1980 ma Agosti 2017, ikiwemo tafiti mpya 45 zilizochapishwa kati ya 2013 na Agosti 2017, maeneo ambayo yameshuhudia vita katika miaka 10 iliyopita yamejumuishwa.

Kwa mujibu wa makadirio hayo kuna takwimu chache kuhusu matatizo ya kuwa na tabia mbili tofauti kuhusu suala moja na wazimuhivyo makadirio kuhusu matatizo haya mawili ya akili yalitokana na makadirio ya kimataifa na hayakujumuisha ongezeko lolote la hatari ya hali hizo katika maeneo ya vita.

Visa viligawanywa katika mafungu matatu, ambayo ni hali mbaya sana, ya wastani na matatizo kidogo, na majanga ya asili pamoja na dharura za umma kama Ebola havikujumuishwa.

Fiona Charlson mwandishi mkuu wa utafiti huu kutoka chou kikuu cha Queensland nchini Australia amesema “Nina imani kwamba utafiti wetu unatoa makadirio sahihi yaliyopo hivi sasa kuhusu hali halisi ya afya ya akili kwenye maeneo ya vita.Tafiti za nyuma zilikuwa zikibadilikabadilika ama zikionyesha kiwango kikubwa zaidu au cha chini zaidi, katika utafiti huu tumetumia vigezo, mikakati na takwimu .”

Maeneo yaliyohusishwa

Hivi sasa kuna migogoro mikubwa ikiwemo ya kibinadamu katika nchi mbalimbali duniani kama vile Afghanistan, Iraq, Nigeria, Somalia, Sudan Kusini, Syria, na Yemen. Mwaka 2016, idadi ya vita vya silaha ilifikia juu kabisa ambapo kulikuwa na migogoro 53 iliyokuwa ikiendelea katika nchi 37 na asilimia 12% ya watu duniani walikuwa wakiishi katika nchi ambazo vita vilikuwa vikiendelea. Karibu watu milioni 69 duniani kote wamelazimika kutawanywa na machafuko na vita  ikiwa ni idadi kubwa kabisa tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia.

Naye Dkt. Mark Van Ommeren kutoka idara ya masuala ya afya ya akili na utumiaji wa mihadarati katika shirika la WHO anasema “makadirio haya mapya pamoja na nyezo ambazo tayari zipo kwa ajili ya kusaidia hali za afya ya akili katika maeneo yenye dharura  vinasisitiza ukweli kwamba kunahitajika haraka uwekezaji wa muda mfupi na endelevu ili huduma ya afya ya akili na msaada wa kisaikolojia viweze kupatikana kwa watu wote wanahitaji ambao wako katika maeneo yaliyoghubikwa na vita au baada ya vita kumalizika.”

Msaada unaotolewa

Dkt. Van Ommeren amehitimisha kwa kusema kwamba katika hali za vita na dharura zingine za kibinadamu WHO inatoa msaada katika njia nyingi, mosi kwa kusaidia uratibu na kutathimini mahitaji ya afya ya akili kwa watu walioathirika, pili kwa kubaini ni msaada gani uliopo mahali hapo na nini zaidi kinahitajika, na tatu kwa kusaidia kujenga uwezo wa msaada mahali ambapo hautoshelezi ama kwa kupitia mafunzo au kutoa rasilimali zaidi.

Pia shirika hilo limesema licha ya athari zilizopo kukiwa na utashi wa kisiasa dharura zinaweza kutumia kujenga huduma bora na endelevu za afya ya akili ambazo zinaendelea kusaidia watu kwa muda mrefu.

Waandishi wa utafiti huo wamesema kuna baadhi ya changamotokutokana na ugumu wa ukusanyaji takwimu katika maeneo ya vitana hii inaanisha kwamba kuna tofauti katika matumizi ya takiwmu zilizotumika na hivyo kuna sintofahamu katika makadirio. Zaidi ya hayo tofauti ya utamaduni katika upimaji na mbadiliko ya mbinu za upimaji vimeathiri makadirio.