Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pigeni marufuku uvutaji wa sigara aina zote shuleni ili kuwalinda vijana – WHO

WHO inasema takriban nusu ya watoto wote duniani wanaripotiwa kupumua hewa iliyochafuliwa na moshi wa tumbaku.
© WHO
WHO inasema takriban nusu ya watoto wote duniani wanaripotiwa kupumua hewa iliyochafuliwa na moshi wa tumbaku.

Pigeni marufuku uvutaji wa sigara aina zote shuleni ili kuwalinda vijana – WHO

Afya

Leo, ili kusaidia kulinda afya ya Watoto, Shirika la Umoja wa Matafa la Afya Ulimwenguni limetoa machapisho mawili mapya, “Uhuru dhidi ya tumbaku na nikotini: mwongozo kwa shule,” na “zana za shule zisizo na nikotini na tumbaku.”

Sekta ya tumbaku inawalenga vijana kwa tumbaku na bidhaa za nikotini na kusababisha matumizi ya sigara ya kielektroniki kuongezeka kwa wavutaji 9 kati ya 10 wanaoanza kabla ya umri wa miaka 18. 

“Bidhaa za tumbaku pia zimefanywa kuwa nafuu kwa vijana kupitia uuzaji wa sigara za kawaida na za umeme na kibaya zaidi haziambatani na maonyo ya kiafya.” Inasema WHO.  

Vishawishi kwa watoto

Shirika hili la afya ulimwenguni linatoa mfano wa hivi karibuni ambapo Mamlaka za usimamizi nchini Marekani mwezi uliopita zimeonya makampuni kuacha kuuza sigara za kielektroniki ambazo zimeundwa kwa mfanano wa vifaa vingine vya shule na hivyo kuwavutia vijana. Pia ziko sigara nyingine zimeundwa kwa muonekano wa vikaragosi au katuni zinazopendwa na watoto au vijana. 

"Iwe kukaa darasani, kucheza michezo nje au kusubiri kwenye kituo cha basi la shule, lazima tuwalinde vijana dhidi ya moshi mbaya wa sigara na utokaji wa sumu ya sigara ya kielektroniki pamoja na matangazo yanayotangaza bidhaa hizi," Dkt Ruediger Krech, Mkurugenzi wa Ukuzaji wa Afya, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni ameonya. 

Mwongozo mpya na zana ni miongozo ya hatua kwa hatua kwa shule kuunda maeneo yasiyo na nikotini na tumbaku, lakini inahitaji mbinu ya "shule nzima" - ambayo inajumuisha walimu, wafanyakazi, wanafunzi, wazazi na kadhalika. Mwongozo na zana ni pamoja na mada kuhusu jinsi ya kusaidia wanafunzi kuacha kuvuta sigara, kampeni za elimu, utekelezaji wa sera na jinsi ya kuzitekeleza.

Njia nne

Mwongozo unaangazia njia nne za kukuza mazingira yasiyo na nikotini na tumbaku kwa vijana:

  • Kupiga marufuku nikotini na bidhaa za tumbaku kwenye maeneo ya shule;
  • Kupiga marufuku uuzaji wa nikotini na bidhaa za tumbaku karibu na shule;
  • Kupiga marufuku matangazo ya moja kwa moja na yasiyo ya moja kwa moja na utangazaji wa nikotini na bidhaa za tumbaku karibu na shule; na kukataa ufadhili au kujihusisha na sekta ya tumbaku na nikotini.
  • Nchi duniani kote ambazo zimeangaziwa katika chapisho hilo kuwa zimetekeleza kwa ufanisi sera zinazounga mkono maeneo ya shule yasiyo na nikotini ikiwa ni pamoja na:

Mwongozo mpya wa WHO unaweza kusaidia kuunda shule zisizo na nikotini na tumbaku ambazo husaidia kuweka watoto wakiwa na afya na usalama. Sera zisizo na nikotini na tumbaku husaidia kuzuia vijana kuanza kuvuta sigara; kuunda mwili wa wanafunzi wenye afya, wenye tija zaidi; kulinda vijana dhidi ya kemikali za sumu katika moshi unaotoka kwa wavutaji wengine; kupunguza uchafu wa sigara; na kupunguza gharama za kusafisha.

Ili kulinda afya ya watu, WHO inahimiza nchi zote kufanya maeneo yote ya umma ya ndani yasiwe na moshi kabisa kulingana na Kifungu cha 8 cha Mkataba wa Mfumo wa WHO wa Kudhibiti Tumbaku.