Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa nafanya kazi kwenye mazingira magumu, sihisi kwa kuwa hii ndoto yangu ya utotoni- Thomas Nyambane

Wakimbizi wa ndani wawili wakiwa wameshikana mikono.Hapa ni Doolow nchini Somalia.
UNOCHA/Giles Clarke
Wakimbizi wa ndani wawili wakiwa wameshikana mikono.Hapa ni Doolow nchini Somalia.

Ingawa nafanya kazi kwenye mazingira magumu, sihisi kwa kuwa hii ndoto yangu ya utotoni- Thomas Nyambane

Msaada wa Kibinadamu

Leo ni siku ya kimataifa ya wasaidizi wa kibinadamu duniani na miongoni mwao ni Thomas Nyambane, Afisa usaidizi wa kibinadamu katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya binadamu na ile ya dharura, UNOCHA nchini Somalia. 

Anatimiza ndoto yake ya utotoni tangu akiwa nchini mwake Kenya kwa kufanya kazi ya kuratibu misaada katika taifa hilo la Pembe ya Afrika. Somalia inapitia kipindi kigumu na inahitaji wahisani na Thomas ni mmoja ya wanaofanikisha hilo. 

1. Je siku hii ya watoa misaada ya kibinadamu ina umuhimu mkubwa kwake? Na je mambo yakoje Somalia?

Kwa kweli nimefanya kazi Somalia kwa zaidi ya miaka 8 na kila kukicha naamka nikiwa na furaha kwani nikiwa mtoto baba yangu alikuwa anazungmza sana kuhusu njaa ya Somalia.

Na nilipojikuta nimeenda huko nilihisi natimiza ndoto yangu ya utotoni hata kama ni nchi ya shida kwa sababu ya vita na mambo ya usalama ni magumu kwa sababu ya makundi yanayowalenga wafanyakazi wa kutoa misaada ya kibinadamu, hivyo huwa tunafanya kazi kwa kuzingatia usalama wetu kabla kuenda kusaidia.

Ijapokuwa ipo changamoto hiyo, nahisi natimiza nia yangu na sihisi kama nafanya kazi hata kama kuna shida ya usalama. Kwa sababu ya hiyo, huwa najikuta nikiwa na wenzangu kutokea mashirika yasiyo ya kiserikali tunashirikiana pamoja na inakuwa rahisi kwani tunafahamu nini tunahitaji kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni za kibinadamu zinazotuongoza na pia kujali usalama wetu kisha kazi inakuwa rahi

2.Siku ya watoa usaidizi wa kibinadamu huadhimishwa tarehe 19 kila Agosti, maudhui ni kwa vyovyote vile, kwako wewe inakuwa hai vipi ukiwa kazini?

Mada ya mwaka huu, kwa vyovyote vile, mimi kama mfanyakazi wa UNOCHA inanilenga binafsi. Kwa kujitolea kwangu kufanya kazi na kuwafikia walioathiriwa vinanifanya nihisi ni siku yangu. Kwanza nasherehekea kama mhudumu wa utoaji wa misaada ya binadamu,pia kutambua ile kazi ina manufaa sio kwangu pekee bali pia kwenye shirika ninalofanya nalo kazi lakini zaidi ya yote walioathiriwa kwa njia mbalimbali na wanahitaji msaada wetu kwa vyovyote vile.