Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

HABARI KWA UFUPI: Dawa za tiba asili, ukatili wa wanamgambo Sudan na madhila Myanmar 

Utumiaji wa dawa za kienyeji ambazo ubora umethibitishwa zinaweza kurahisisha kutoa huduma za afya, hasa katika maeneo ya vijijini ambayo mifumo ya kawaida ya huduma za afya ni duni. Dawa asilia zenye ubora inaweza kuwa faida kwa idadi kubwa ya watu kwan…
WHO/Ernest Ankomah
Utumiaji wa dawa za kienyeji ambazo ubora umethibitishwa zinaweza kurahisisha kutoa huduma za afya, hasa katika maeneo ya vijijini ambayo mifumo ya kawaida ya huduma za afya ni duni. Dawa asilia zenye ubora inaweza kuwa faida kwa idadi kubwa ya watu kwani ndiyo chanzo kikuu au hata chanzo pekee cha huduma za afya kwa takriban 80% ya watu barani Afrika.

HABARI KWA UFUPI: Dawa za tiba asili, ukatili wa wanamgambo Sudan na madhila Myanmar 

Masuala ya UM

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus leo mjini Gandhinagar jimboni Gujarat nchini India amefungua mkutano wa kwanza wa shirika hilo kuhusu dawa za tiba asili akisema wanasaka Ushahidi wa pamoja na data za kuruhusu matumizi salama ya tiba ya aina hizo huku akisema dawa hizo ni kimbilio la kwanza kwa mamilioni ya watu duniani kote na kwamba wanapanga ikiwezekana mkutano huu uwe ufanyika kila baada ya miaka miwili.  

SUDAN 

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa leo wameelezea kusikitishwa na ripoti za matendo ya kikatili na kuenea ya ubakaji na aina nyinginezo za unyanyasaji wa kingono unaofanywa na wanamgambo waasi wa kikundi cha Rapid Support Forces (RSF) wakati wa mzozo wa ndani uliodumu kwa miezi minne sasa katika Jamhuri ya Sudan. Wataalamu hao wametoa wito wa kukomeshwa vurugu zinazoendelea.  

MYANMAR 

Na Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu ambaye pia ni Mkuu wa ofisi ya kuratibu masuala ya dharura na misaada ya kibinadamu OCHA, Martin Griffiths leo akihitimisha ziara ya siku tatu nchini Myanmar ametoa wito wa kuongezwa kwa huduma za kibinadamu na ufadhili kusaidia watu milioni 18 wanaohitaji msaada kote nchini humo.