Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Je, yapi maoni yako kuhusu huduma zinazotolewa na UN News?

Hojaji ya mtumiaji ya UN News Kiswahili
UN News
Hojaji ya mtumiaji ya UN News Kiswahili

Je, yapi maoni yako kuhusu huduma zinazotolewa na UN News?

Masuala ya UM

Huduma ya habari ya vyombo vya habari vya Umoja wa Mataifa (UN News) imezindua hojaji mpya mtandaoni ili kupata maoni kutoka kwa wasomaji, wasikilizaji na watazamaji wake kusikia nini maoni yako kuhusu huduma yetu, na jinsi tunavyoweza kuhudumia mahitaji yako vyema.

Hojaji yetu ya maoni itakayochukua dakika 4 tu mtandaoni yenye maswali 12 itatusaidia kuboresha matumizi yako kwenye tovuti hii ya kompyuta za mezani na simu ya mkononi au ya rununu, na kutusaidia kuelewa tunachohitaji kufanya zaidi, au kupunguza.

Huduma ya Habari ya Umoja wa Mataifa huwapa mamilioni ya watu ulimwenguni kote habari za kila siku za Umoja wa Mataifa kupitia habari za papo kwa papo, mahojiano, makala za kina na mengine mengi.

Utafiti wetu wa awali wa mwaka 2021 ulisaidia kukusanya maoni kutoka kwa maelfu ya watumiaji na kusababisha uboreshaji mkubwa wa tovuti ya Habari za UN.

Mwezi huu tunaomba maoni zaidi ili kufanya maboresho zaidi. Tufahamishe jinsi tunavyofanya,  kile unachopenda na wapi tunaweza kuhitaji kuongeza mambo.

Hivi karibuni tulitangazwa washindi wa tuzo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2022 kwa kutoa huduma kwa lugha nyingi, lakini tumeazimia kutobweteka.

Tunataka kuboresha bidhaa na huduma zetu kwa ajili yenu, wasomaji wetu, wasikilizaji na watazamaji wetu. Tafadhali fanya jaza hojaji hii mtandaoni kwa dakika 4, yenye maswali 12 bila kutambulisha majina yako ili kusaidia UN News kuhudumia mahitaji yako ya habari vyema.

Hojaji hii iko karika lugha zote 9 ambazo Habari za UN inazitumia, tafadhali bofya kwenye link hii ujaze hojaji hiyo.