Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takriban watu 23 wameuawa katika maandamano Kenya, hii haikubaliki: OHCHR

Geti la kuingia kwenye makao makuu ya ofisi ya haki za binadamu OHCHR mjini Geneva Uswis
UN Photo/Jean-Marc Ferré
Geti la kuingia kwenye makao makuu ya ofisi ya haki za binadamu OHCHR mjini Geneva Uswis

Takriban watu 23 wameuawa katika maandamano Kenya, hii haikubaliki: OHCHR

Haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR leo imesema ina toiwa hofu kubwa na kusambaa kwa ghasia na madai ya kutumia nguvu kupita kiasi kunakofanywa na polisi ikiwemo matumizi ya risasi za moto wakati wa maandamano nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi hiyo iliyotolewa mjini Geneva Uswisi ripoti zinasema takriban watu 23 wameuawa na wengine kwa makumi kujeruhiwa katika maandamano ya wiki iliyopita.

Ofisi hiyo ya haki za binadamu imetoa wito wa kufanyika haraka na kwa kina uchunguzi huru na wa wazi dhidi ya vifo hivyo na majeruhi.

Msemaji wa OHCHR Jeremy Laurence amesema “Wale wote waliohusika na mauaji na majeruhi hao lazima wawajibishwe nah atua Madhubuti za kuzuia vifi zaidi na majeruhi lazima zichukuliwe.”

Pia amesema, "Kutokana na wito wa maandamano zaidi wiki ijayo, tunatoa wito kwa mamlaka kuhakikisha haki ya kukusanyika kwa amani kama inavyothibitishwa na katiba ya Kenya na sheria za kimataifa za haki za binadamu. Ulinzi wa mikusanyiko lazima utafute kuwezesha mikusanyiko ya amani, na matumizi yoyote ya nguvu lazima yaongozwe na kanuni za uhalali, ulazima, uwiano na kutobagua. Silaha za moto hazipaswi kamwe kutumiwa kutawanya mikusanyiko.”

Ameendelea kusema kuwa "Tunatoa wito wa kuwepo kwa utulivu na kuhimiza mazungumzo ya wazi ili kushughulikia malalamiko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa, kwa lengo la kupata suluhu ya kudumu kwa maslahi ya Wakenya wote."