Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS kuzindua ripoti yake ya Njia Inayomaliza UKIMWI

UNAIDS kuzindua ripoti ya Njia Inayomaliza UKIMWI
Photo: UNAIDS
UNAIDS kuzindua ripoti ya Njia Inayomaliza UKIMWI

UNAIDS kuzindua ripoti yake ya Njia Inayomaliza UKIMWI

Haki za binadamu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kukotokomeza Virusi vya Ukimwi na UKIMWI (UNAIDS) limeeleza leo kwamba wiki ijayo tarehe 13 Julai 2023 litazinduataarifa mpya ya ripoti yake ya mwaka 2023 kuhusu UKIMWI Ulimwenguni. 

 

 

Taarifa ya leo inadokeza kuwa ripoti yenye jina Njia Inayomaliza UKIMWI  inaeleza kuwa ingawa kuna changamoto nyingi kuelekea njia ya kumaliza kabisa virusi vya UKIMWI na ugonjwa wa UKIMWI ulimwenguni, lakini kuna nchi nyingi zimeonesha suala hili linawezekana iwapo kuna utashi wa kisiasa.

Aidha ripoti hiyo inafafanua kuwa inaposema utashi wa kisiasa inamaanisha kutoa ufadhili wa kutegemewa na wa kutosha; kufuata takwimu na ushahidi; kupunguza kukosekana kwa usawa na ubaguzi unaonyima huduma za watu, kutumia zana za kisayansi zinazolinda ustawi, na kipengele muhimu cha kutambua na kushirikisha afua zinazoongozwa na jamii.

Njia Inayokomesha UKIMWI

Vilevile ripoti hiyo imeangazia maeneo yenye utofauti mkubwa sana, ambapo imejumuisha ahadi za kisiasa, njia zinazo zingatia haki za binadamu ili kusaidia watu wanaoishi na walioathirika na VVU, na kubaini kuna maendeleo ya kuvutia katika kupunguza maambukizi mapya ya VVU na vifo vinavyohusiana na UKIMWI.

Hata hivyo ripoti hiyo inatanabaisha kuwa wakati viongozi wanapopuuza, kuwatenga na kuwafanya kuwa wahalifu watu wanaoishi, au walio katika hatari ya VVU, maendeleo katika mwitikio wa UKIMWI yanazuiwa, huku watu wengi zaidi na zaidi wakiendelea kuambukizwa Virusi vya UKIMWI-VVU.