Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiswahili ni daraja baina ya Afrika na Dunia UNESCO inaungana na Afrika kuienzi:Estelle Zadra

Estelle Zadra, Afisa Uhusiano wa ofisi ya UNESCO akihojiwa na Flora Nducha.
UN News/Kiswahili
Estelle Zadra, Afisa Uhusiano wa ofisi ya UNESCO akihojiwa na Flora Nducha.

Kiswahili ni daraja baina ya Afrika na Dunia UNESCO inaungana na Afrika kuienzi:Estelle Zadra

Utamaduni na Elimu

Maadhimisho ya pili ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani yatafanyika wiki ijayo Julai 7 na sasa maandali zi yanafanyika katika kila kona kuhakikisha siku hiyo iliyopewa uzito mkubwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO lakini pia inatumika kama jukwaa la kuziunganisha jamii sio za Afrika tu zinazozungumza Kiswahili ali na nyinginezo zinazokumbatia Kiswahili.

Estelle Zadra Afisa Uhusiano wa ofisi ya UNESCO hapa New York. ameeleza kwamba kuna mambo mengi yatakayojiri siku hiyo, “Kuanzia hapa New York hadi Paris, Dar es salaam hadi Nairobi na katika miji mbalimbali ya Afrika tutakuwa na mijadala na matukio ya kitamaduni ili kuwafanya washiriki kuwa sehemu ya lugha hii iliyosheheni ya Kiswahili. Mbali ya matukio ya kijamii kama mazungumzo na mijadala tutakuwa na hafla mbalimbali za kitamaduni, kama dansi, muziki na hata chakula cha kitamaduni.”

Hata hivyo nilitaka kufahamu nini maudhui ya mwaka huu na kwanini wameyachagua hayo Etelle hakutafuna maneno, “Kiswahili ni lugha ya umoja na mawasiliano kwa watu wengi sana barani Afrika na nje ya Afrika lakini tunataka kuonyesha kwa jinsi gani Kiswahili kilivyo na uwzekao mkubwa katika zama za kidijitali, hivi sasa jamii zetu zimeunganishwa sana na ni muhimu kila mtu kuwa na fursa ya nyenzo hizo na tunazihitaji kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na mijadala katika jamii zetu na kila mtu kushiri hivyo maudhui ya mwaka huu ni “Kuibua uwezo wa Kiswahili katika zama za kidijitali kwa sababu tunauhakika kwamba Kiswahili kinaweza kutumika kama daraja kuunganisha jamii mbalimbali na kuwezesha ujumuishwaji katika ulimwengu wa kidijitali.”

Na ili kuhakikisha maudhui haya yanatimia Estelle amesema wanashirikiana kwa karibu n anchi zote za Afrika Mashariki na za Jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa afrika SADC  ambazo pia zimekikumbatia Kiswahili lakini pia amesema lengo kuu ni kuwafikia vijana hususan wajasiriamali ambao wana hamu ya kutumia nyenzo za kidijitali kujiendeleza na lugha mujarabu kwao ni Kiswahili . Na mwisho Estelle akasema ujumbe wa UNESCO kwa dunia kuhusu siku hii ni kwamba,  “Kiswahili sio lugha tu bali ni mkusanyiko mahiri wa urithi uliosheheni wa kitamaduni wa Afrika Mashariki na tunadhani kwa kukumbatia Kiswahili katika zama za kidijitali tunatoa fursa ya kubadilishana utamaduni, kuchagiza ukuaji wa uchumi na uwezeshaji wa kielimu. “ 

Siku ya lugha ya Kiswahili duniani
UN News
Siku ya lugha ya Kiswahili duniani

Siku ya lugha ya kiswahili duniani huadhimishwa kila mwaka tareje 7 Julai tangu ilipopitishwa rasmi na UNESCO miaka mwili iliyopita.