Yoga ni kiungo cha maisha na ubinadamu wetu: Guterres
Yoga ni kiungo cha maisha na ubinadamu wetu: Guterres
Ikiwa leo ni siku ya Yoga duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “Yoga ni kiungo, inaunganisha mwili na akili, ubinadamu na asili na mamilioni ya watu kote ulimwenguni, ambao kwao ni chanzo cha nguvu, maelewano, na amani.”
Katika ujumbe wake maalum wa siku hii mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa “Katika ulimwengu hatari na uliogawanyika, manufaa ya mazoezi hayo ya kale ni ya thamani sana. Yoga inatoa fursa ya utulivu, inaweza kupunguza wasiwasi na kukuza ustawi wa akili.”
Pia amesema yoga “Inatusaidia kuboresha nidhamu na subira. Inatuunganisha na sayari yetu, ambayo inahitaji sana ulinzi wetu. Na inafichua ubinadamu wetu wa kawaida ili kutusaidia kuelewa kwamba licha ya tofauti zetu, sisi ni wamoja.”
Na hivyo ametoa wito maalum “Katika siku hii ya kimataifa ya Yoga, hebu tukumbatie roho ya umoja, na tuazimie kujenga ulimwengu bora na wenye usawa kwa watu, sayari na sisi wenyewe.”
Siku ya kimataifa ya yoga huadhjimishwa kila mwaka Juni 21 katika sehemu mbalimbali duniani na mwaka huu hapa kwenye Umoja wa Mataifa kutakua na hafla maalum ya mazoezi ya Yoga itakayoendeshwa na waziri mkuu wa India Narendra Modi kuadhimisha siku hii.
Maudhui ya siku ya yoga mwaka huu ni “Yoka kwa ajili ya Vasudhaiva kutumbkam” ikimaanisha “Yoga kwa ajili ya ustawi wa sayari moja, familia moja.”