Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinda amani wa Tanzania nchini CAR awafanya tathmini ya miradi kwa wananchi

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania (TANBAT 6) kinachohudumu chini ya MINUSCA wafanya tathmini ya miradi kwa wananchi CAR.
TANBAT 6/Kapteni Mwijage Inyoma
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania (TANBAT 6) kinachohudumu chini ya MINUSCA wafanya tathmini ya miradi kwa wananchi CAR.

Walinda amani wa Tanzania nchini CAR awafanya tathmini ya miradi kwa wananchi

Amani na Usalama

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania (TANBAT 6) kinachohudumu chini ya MINUSCA wametembelea miradi mbalimbali ya wananchi ikiwa ni kwa ajili ya kufanya tathmini ya maendeleo ya miradi ambayo wanajeshi hao waliwaanzishia wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR. 

Kwanza walinda amani hawa kutoka Tanzania wameanzia kwenye shamba la mahindi na kumkuta mwenyekiti wa Kikundi cha vijana waliofundishwa kulima kwa kutumia jembe la mkono na pia kupewa mbegu za mahindi Mamaduu Daneil ambaye anaeleza mikakati waliyonayo baada ya kupewa mtaji wa elimu ya kilimo kutoka TANBAT 6. 

"kama unavyoona mahindi yamestawi vizuri baada ya kuelekezwa na ndugu zetu walinda Amani toka Tanzania tunamshukuru sana MINUSCA Kwa walinda amani wake wanavyo shiriki kutupa elimu za shughuli za maendeleo." Anasema Mamaduu Daneil. 

Hawakuishia hapo walinda amani hao pia wakazindua mradi wa ufugaji samaki kwa kikundi cha wazee ambapo wawapatia mbegu ya vifaranga vya samaki zaidi ya mia sita. Mkuu wa kikundi hicho Franco Christopher anatoa shukrani zake kwa MINUSCA akisema,"Shukrani zetu ziwafikie walinda amani kwa jinsi wanavyozidi kushiriki na sisi katika maendeleo. Na mkuu wao Luteni Kanali Amini Stephen Mshana tunamshukuru kwa kutupa mtaji mkubwa wa kutusaidia kujipatia kipato, tunaahidi kuendeleza vizuri mradi huu.” 

Baada ya kujiridhisha na juhudi zinazoendelea na vikundi hivyo wakaweka pia jiwe la msingi kama ishara ya kuanza usimamizi wa ujenzi wa daraja la barabara ya mji wa Nasole ambayo ilikuwa imeharibika na haipitiki kabisa  ambapo Meya wa mji huo (kama una jina lake litaje hapa) katika hafla hiyo anashukuru TANBAT6 chini ya MINUSCA akisema, "Wanakijiji cha Nasole wamepata shida katika kusafiri wa vyombo vya moto na wakati mwingine hata kwa miguu. Wagonjwa walipata shida kutoka kijiji jirani kuja huku kupata matibabu kwa sababu ya kukosa barabara  lakini leo Tanzania chini ya MINUSCA wameamua kusimamia kutengeneza daraja hili kuungana njia na kurahisisha usafiri. Asanteni sana Tanzania" 

Na kama walivyonena wahenga baada ya dhiki faraja, sherehe na shangwe vikafuata katika viwanja vya mji wa Nasole kwa walinda amani walio chini ya MINUSCA kwa kushirikiana na uongozi wa Beriberati, Mambéré-Kadéï.