Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Akiwa Jamaica, Katibu Mkuu wa UN azungumzia mshikamano na kutaja vikwazo vya maendeleo

Katibu Mkuu wa UN António Guterres (kulia) akishikana mkono  na Waziri Mkuu wa Jamaica Andrew Holness  kabla ya mkutano wao na waandishi wa habari mjini Kingston, Jamaica
Picha ya UN /Jermaine Duncan 
Katibu Mkuu wa UN António Guterres (kulia) akishikana mkono na Waziri Mkuu wa Jamaica Andrew Holness kabla ya mkutano wao na waandishi wa habari mjini Kingston, Jamaica

Akiwa Jamaica, Katibu Mkuu wa UN azungumzia mshikamano na kutaja vikwazo vya maendeleo

Ukuaji wa Kiuchumi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres  ameelezea mshikamano wa dhati na Jamaica na mataifa mengine ya visiwa vidogo yanayoendelea akibainisha kile alichosema kuwa ni changamoto za kimaadili, kimadaraka ambazo zinakwamisha mfumo wa sasa wa fedha duniani kusaidia maendeleo endelevu sawia duniani.

Amesema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari huko Kingston, Jamaica, mkutano uliohudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa taifa hilo Andrew Holness akieleza “tumeazimia kufanyia marekebisho na hii ndio sababu ya ziara yangu.”

Bwana Guterres amesema katika mazungumzo yake na Waziri Holness wamejadili “hali ya kutisha” nchini Haiti, akisema hiyo ilikuwa changamoto kubwa ya kisiasa inayokabili ukanda mzima wa Karibea, akipongeza ushiriki wa Jamaica katika kusaka suluhu ya haraka ya janga hilo, sambamba na ushiriki wa chombo cha kikanda kinachohusisha mataifa 15 ya eneo hilo, CARICOM.

Uvamizi kwa amani

Amepongeza uwezo wa Jamaica wa “kuvamia kwa amani dunia nzima kupitia utamaduni, muziki na sanaa yake,” kwa miongo ya hivi karibuni, ikithibitisha kuwa utofauti baada ya ukoloni, unaweza kuwa utajiri na si kitisho, alimradi sera sahihi zinapitishwa.

“Leo hii – tunapotazama muundo wa sasa wa mfumo wa fedha duniani – tatizo la kimaadili, tatizo la madaraka na tatizo lililoko wazi,” amesema Katibu Mkuu.

Kuhusu maadili, amekumbusha kuwa utengenezaji wa chanjo dhidi ya coronavirus">COVID-19, usambazaji na kujikwamua baada ya gonjwa hilo, umedhibitiwa zaidi na nchi tajiri, ambazo zina uwezo wa kuchapisha noti za fedha, ilhali nchi zinazoendelea hazikuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Amerejelea suala la changamoto za uwepo wa rasilimali nyingi duniani ambamo kanuni zilizopindishwa za kimataifa inamaanisha ukosefu wa haki unajengewa mfumo, huku nchi zenye maendeleo duni zikisalia kutegemea kuonewa huruma na mifumo ya ukopeshaji imepitwa na wakati na sio ya haki.

Katibu Mkuu wa UN António Guterres (wa tatu kushoto) akivutiwa na kazi ya sanaa kwenye ushoroba wa sanaa, huko Water Lane mjini Kingston, Jamaica ambako yuko kwa ziara rasmi.
Picha ya UN/Jermaine Duncan
Katibu Mkuu wa UN António Guterres (wa tatu kushoto) akivutiwa na kazi ya sanaa kwenye ushoroba wa sanaa, huko Water Lane mjini Kingston, Jamaica ambako yuko kwa ziara rasmi.

Waathirika wa tabianchi

“Nchi za visiwa vidogo zinazoendelea ziko hatarini zaidi kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi zaidi kwa sababu ya mfumo wa uchumi wao, eneo ambamo ziko na ukubwa wao,” amesema Katibu Mkuu.

Pili, ametaja mifumo ya mamlaka iliyoanzishwa huko Bretton Woods, baada ya kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, wakati ambao nchi kama Jamaica zilikuwa bado chini ya himaya ya Uingereza, hazina sauti yoyote, halikadhalika nchi nyingi za Afrika.

“Na ni dhahiri, mifumo iliyoanzishwa imedhihirisha uhusiano wa kimamlaka uliokuweko baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Imepitwa na wakati, na hivyo mifumo hiyo si ya haki na haifanyi kazi. Mfumo huo unapaswa kurekebishwa ili uendane na hali ya sasa ya uchumi duniani.”

Na sasa, ameongeza kuna changamoto dhahiri kuelekea maendeleo endelevu na sawia.

“Na mengi zaidi yanaweza kufanywa kwenye kuweka uhusiano bora kati ya tabianchi nchi na ufadhili na usaidizi thabiti kwenye kujenga mnepo, hasa kwa nchi za visiwa vidogo zinazoendelea.”

Kujenga mfumo ulioharibika

Katibu Mkuu amesema hatua nyingi zaidi zinaweza kuchukuliwa kwa kusambaza faida za majukumu ya benki za kimataifa, iwapo zitabadili miundo yao ya biashara – na zina uwezo wa kutumia rasilimali ili kuongeza fursa za nchi zinazoendelea kupata mikopo binafsi kwa gharama nafuu.

Katibu Mkuu amesema atahutubia mkutano wa kundi la nchi 7 G7, wiki hii na kundi la nchi 20, G20 litakapokutana tena na atasisitiza kushughulikiwa kwa kina hoja za maadili, mamlaka na utendaji.

Amemwelezea Bwana Holness kama bingwa kwenye kuchukua hatua dhidi ya tabianchi na bingwa pia kuhusiana na mfumo fanisi uliorekebishwa duniani.

Kuokoa mustakabali wa Haiti

Kuhusu Haiti, Bwana Guterres amesema majanga lukuki yatokanayo na ghasia za magenge yaliyojhami, mfumo wa kisiasa uliolemaa, machungu ya kibinadamu na ukosefu wa usalama vinataka ahadi thabiti kutoka jamii ya kimataifa.

Amekumbusha pendekezo lake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo bado halijazingatiwa la kutaka kuweko kwa polisi bora wa kimataifa ili kuendesha msako dhidi ya magenge ya uhalifu sambamba na mchakato wa kisiasa, na kuweka mazingira ya kutatua hali iliyoko.

Jamaica imeahidi kubeba wazo hilo sambamba na CARICOM inawekeza katika kujaribu kuleta pamoja wadau wa Haiti ili kusaka suluhu.

“Nataka kuelezea uungaji wangu mkono wa hatua za Jamaica na CARICOM. Na nataka kwa mara nyingine tena, kuisihi jamii ya kimataifa ielewe mshikamano fanisi na Haiti sio tu ni suala la ukarimu, bali ni muhimu kwa sababu hali ya sasa Haiti inaakisi kitisho cha usalama kwenye ukanda mzima na maeneo mengine duniani..