Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP inaanza mara moja operesheni zake Sudan baada ya kuzisitisha kwa muda: McCain

WFP katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka huu imelisha wakimbizi 387,000 nchini Sudan.
WFP/Belinda Popovska
WFP katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka huu imelisha wakimbizi 387,000 nchini Sudan.

WFP inaanza mara moja operesheni zake Sudan baada ya kuzisitisha kwa muda: McCain

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limesema linarejelea mara moja operesheni zake za msaada wa kibinadamu nchini Sudan baada ya kuzisitisha kwa muda wafanyakazi watatu wa shirika hilo walipouawa Aprili 15 mwaka huu.

Katika taarifa yake iliyotolewa mjini Roma Italia hii leo mkurugenzi mtendaji wa WFP Cindy McCain amesema ugawaji wa chakula unatarajiwa kuanza katika siku chache zijazo kwenye majimbo ya Gedaref, Gezira, Kassala na White Nile kwa lengo la kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa maelfu ya watu ambao wanauhitaji msaada huo kwa udi na uvumba.

Bi. McCain amesema mgogoro unaoendelea nchini Sudanunawssukuma mamilioni ya watu katika janga la njaa  na hali ya usalama bado ni tete.

Mkuu huyo wa WFP amesema pamoja na kuwa wanaanza tena operesheni zao lakini wanafikiria kwa makini maeneo ambayo wana fursa ya kuyafikia lakini pia suala la usalama, uwezo wao na masuala mingine ya muhimu ya ufikiaji.

“Tutachukua kila tahadhari kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wetu na washirika wetu wakati tukikimbizana kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya watu walio hatarini zaidi.”

Amesisitiza Bi. McCain na kuongeza kuwa “Ili kuwalinda vyema wahudumu wetu wanaohitajika sana na watu wa sudan mapigano lazima yakome.”

Zaidi ya watu milioni 15 walikuwa wanakabiliwa na hali mbayá ya kutokuwa na uhakika wa chakula Sudan hata kabla ya kuanza kwa mgogoro wa sasa.

Mkuu huyo wa WFP amehitimisha taarifa yake kwa kusema kuwa “Tunatarajia idadi hii kuongezeka kwa kiasi kikubwa n ani wakati kama huu ambapo WFP na washirika wake wa Umoja wa Matifa wanapohitajika sana.”

UN kutuma kigogo Sudan

Kufuatia hali ya kibinadamu kuendelea kuzorota nchini Sudan Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema anamtuma mara moja mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya misaada ya dhrura na mkuu wa masuala ya kibinadamu Martin Griffiths kwenye kwenye ukanda huo.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo mjini New Yory Marekani Guterres amesema “Kiwango na kasi ya kinachoendelea nchini Sudan si yakawaida. Tuna hofu kubwa ya athari za sasa na za muda mrefu kwa watu wote nchini Sudan na maeneo ya karibu.Kwa mara nyingine tunatoa wito kwa pande zote katika mzozo huo kuwalinda raia na miundombinu ya raia, kuruhusu raia wanaokimbia mapigano kupita kwa usalama , kuheshimu wahudumu wa kibinadamu na mali zao, kuwezesha operesheni za misaada na kuheshimu wahudumu wa afya, usafiri na vituo vyao.”

Vita imepandisha bei ya chakula na mafuta

Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limesema mapigano yanayoendelea nchini Sudan baina ya vikosi vya serikali na vikos vvya msaada wa haraka SAF ymeleta na yanaendelea kusababisha athari kubwa kwa raia.

Athari hizo ni pamoja ya ongezeko kubwa la bei za chakula, mafuta na bidhaa zingine za msingi na hivyo kufanya watu wengi kutomudu gharama za bidhaa muhimu.

Pia shirika hilo limesema idadi ya raia wanaokimbia machafuko inaendelea kuongezeka wengi wakikimbilia nchi jirani za Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Chad, Ethiopia, Misri, Saudia na Sudan Kusini.

Changamoto nyingine kubwa kwa mujibu wa OCHA ni uporaji wa mali za huduma za misaada ya kibinadamu na ofisi zao hasa katika maeneo muhimu ya utoaji misaada.

Na sasa juhudi zinafanyika ili kufikisha msaada wa kibinadamu pale inapowezekana.