Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres: Suriname msifanye maandamano ya vurugu

Msongamano wa magari katika jiji la Paramaribo, Suriname.
Unsplash
Msongamano wa magari katika jiji la Paramaribo, Suriname.

Guterres: Suriname msifanye maandamano ya vurugu

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ana wasiwasi na maandamano ya vurugu yaliyotokea nchini Suriname tarehe 17 mwezi huu wa Februari, 2023 ambapo majengo ya bunge yalivunjwa, mali ya watu binafsi kuharibiwa na watu wengi kujeruhiwa.

Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa Katibu Mkuu Stéphane Dujarric imesema ni vyema wananchi wakazingatia kuteleza haki zao lakini kwa amani pasi na vurugu

“Katibu Mkuu anasisitiza kuwa uhuru wa kujieleza na kukusanyika kwa amani ni haki za msingi za binadamu zinazopaswa kuheshimiwa wakati wote, lakini maandamano lazima yafanyike bila kutumia vurugu.”

Dujarric amesisitiza kuwa Katibu Mkuu anawataka wahusika wote nchini Suriname kujizuia, na kushiriki katika mazungumzo jumuishi ili kutatua changamoto zinazoikabili nchi hiyo kwa njia inayojenga na si kubomoa.