Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima tumakinike zaidi asema Guterres katika siku ya kuzuia machafuko ya itikadi kali

Nchi nyingi zinaendelea kukabiliwa na matishio ya ugaidi.
UNODC
Nchi nyingi zinaendelea kukabiliwa na matishio ya ugaidi.

Lazima tumakinike zaidi asema Guterres katika siku ya kuzuia machafuko ya itikadi kali

Amani na Usalama

Wakati makundi yenye itikadi kali yakipanua wigo wao, jumuiya ya kimataifa haiwezi kuacha tahadhari yake dhidi ya ugaidi, amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres 

Wito huo umekuja katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya Kuzuia machafuko yatokanayo na misimamo mikali ikiwa ni kwa mara ya kwanza kabisa maadhimisho hayo yanafanyika na wakati unaofaa baada ya kupitishwa  mwezi Desemba na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Bwana Guterres ameelezea kuwa “Ugaidi ni dharau kwa ubinadamu kwani unadhoofisha maadili yanayotuunganisha pamoja.”

Pia amesema ugaidi unatishia juhudi za pamoja za kukuza amani na usalama, kulinda haki za binadamu, kutoa misaada ya kibinadamu, na kuendeleza maendeleo endelevu.

Ardhi yenye rutuba kwa chuki

"Lazima tuwe waangalifu zaidi kuliko hapo awali," amesema, akibainisha kuwa "makundi ya kigaidi na yenye itikadi kali yanapata ardhi yenye rutuba kwenye mtandao ili kutema sumu yao mbaya."

Ameongeza kuwa vuguvugu la Unazi-mamboleo, la itikadi kali za watu weupe linazidi kuwa hatari siku hadi siku na sasa linawakilisha tishio la juu zaid la usalama wa ndani katika nchi kadhaa, pamoja na kuongezeka kwa kasi zaidi.

Kuzuia na kujumuishwa

Katibu Mkuu amehimiza kwamba “nchi lazima zichukue hatua ili kukabiliana na changamoto hiyo kwa kuzuia, na kwa kushughulikia hali za msingi zinazochochea ugaidi kwanza.”

Pia amesisitiza umuhimu wa ujumuishaji na kuhakikisha kuwa mikakati ya kukabiliana na ugaidi inaakisi sauti mbalimbali hasa walio wachache, wanawake na vijana.

Haki za binadamu lazima ziwe msingi wa sera zote za kukabiliana na ugaidi, aliongeza. Amesema .

Amehitimisha ujumbe wake kwa wito kwamba "Leo na kila siku, tushirikiane kujenga jamii zenye amani zaidi, umoja na utulivu ambamo ugaidi na itikadi kali havina makao."