Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pelé alikuwa mwenye roho nzuri anayependa watoto – Wanafamilia

[Kushoto kwenda kulia] karibu na mpira wa soka ni Katibu Mkuu wa zamani wa UN Kofi Annan, nyota wa soka wa Brazil Pele na Rais wa FIFA Joseph Blatter katika mkutano na waandishi wa habari wakitangaza uamuzi wao wa kujiunga katika uhusiano wa ushirika FIF…
UN Photo/Eskinder Debebe
[Kushoto kwenda kulia] karibu na mpira wa soka ni Katibu Mkuu wa zamani wa UN Kofi Annan, nyota wa soka wa Brazil Pele na Rais wa FIFA Joseph Blatter katika mkutano na waandishi wa habari wakitangaza uamuzi wao wa kujiunga katika uhusiano wa ushirika FIFA kuipigia debe United Nati

Pelé alikuwa mwenye roho nzuri anayependa watoto – Wanafamilia

Utamaduni na Elimu

Ulimwengu umeendelea kuomboleza kwa masikitiko kifo cha mcheza soka wa Brazil Edson Arantes do Nascimento, almaarufu Pelé. Kwa Umoja wa Mataifa Pelé alikuwa mshambuliaji muhimu katika kufanikisha ushindi wa malengo ya Umoja wa Mataifa.

Kwa nyakati tofauti aliteuliwa kuwa Balozi Mwema wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kama elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO na kuhudumia watoto UNICEF. UN News kupitia Idhaa ya Kireno imepata fursa ya kuzungumza na mtoto wake wa kiume na mkewe kuhusu Pelé nje ya uwanja.

Ni Monica Grayley wa Idhaa ya Kireno ya Umoja wa Mataifa akimkaribisha Joshua Nascimento mmoja wa watoto wa kiume wa Pelé. Na baada ya mazungumzo kuhusu namna Pelé alivyowalea kwa adabu japo bila kuwaadhibu sana, swali likawa…ni kwa namna gani ungependa baba yako akumbukwe kwa vizazi vingi vijavyo?

Joshua Nascimento anajibu kuwa angependa baba yake kwanza akumbukwe kama mchezaji bora kama alivyokuwa wakati wake na mafanikio yote aliyokuwa nayo kwa mchezo huo lakini pia mambo aliyoyafanya nje ya mchezo, mambo aliyoyafanya kwa nchi yake ya Brazil na hasa kwa watoto hata pale alipofunga goli lake la 1000 alisema ni kwa ajili ya kuwajali watoto.

Kijana Joshua alikuwa akiyasema haya akiwa ameketi na mama yake mzazi, Assiria Lemos, mke wa zamani wa Pele naye anajibu swali kama hilo la Je, angependa Pelé akumbukwe vipi? Anasema ukiacha kile ambacho kila mtu anakifahamu kuwa Pele alikuwa mcheza mpira wa miguu wa kiwango cha juu, lakini pia kama mtu tu binafsi alikuwa,“mstahimilivu, mnyenyekevu, mkarimu, mwenye roho nzuri, mtu wa familia anayejali watu wa familia yake na watu wenye uhitaji. Roho nzuri.”