Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jaji Mohamed Chande Othman wa Tanzania ateuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Haki za Binadamu Ethiopia

Jaji Mohamed Chande Othman wa Tanzania ateuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Haki za Binadamu Ethiopia
UN News
Jaji Mohamed Chande Othman wa Tanzania ateuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Haki za Binadamu Ethiopia

Jaji Mohamed Chande Othman wa Tanzania ateuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Haki za Binadamu Ethiopia

Haki za binadamu



Rais wa Baraza la Haki za Binadamu, Balozi Federico Villegas (Argentina), amemteua Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mohamed Chande Othman kuwa Mjumbe wa Tume na Mwenyekiti wa Tume ya Wataalamu wa Haki za Binadamu nchini Ethiopia.

Taarifa iliyotolewa Jumatano hii tarehe 21 Desemba 2022 mjini Geneva Uswisi imeeleza kuwa Uteuzi wa Bwana Othman unakuja kufuatia kujiuzulu kwa Kaari Betty Murungi kama Mwenyekiti na Mjumbe wa Tume. Balozi Villegas amemshukuru Bibi Murungi kwa jukumu lake katika Tume na amemtakia kila la kheri katika shughuli zake zijazo.


Bwana Othman aiyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania kuanzia mwaka 2010 hadi 2017, aliwahi kuteuliwa na aliyekuwa wakati huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki-moon mwaka 2015 kuwa Mwenyekiti wa Jopo Huru la Wataalamu wa Uchunguzi wa kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld. Mnamo 2019-2020, Bwana Chande Othman alihudumu kama mjumbe wa Mapitio ya Mtaalam Huru ya  Mahakama ya Kimataifa ya Jinai na Mfumo wa Mkataba wa Roma (ulioanzisha ICC), baada ya kuteuliwa na Bunge la Nchi Wanachama wa Mkataba wa Roma wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.


Uzoefu wa awali wa Bwana Othman unajumuisha ule wa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Timor-Leste (2000-2001), Mkuu wa Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Rwanda (1998-2000), na Mshauri Mkuu wa Sekta ya Sheria na Haki wa UNDP-Cambodia. Pia amewahi kuwa mjumbe wa Tume ya Ngazi ya Juu ya Baraza la Haki za Kibinadamu la Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu Hali nchini Lebanon kufuatia Mzozo wa Silaha wa Israel na Lebanon mwaka 2006 na kama Mtaalam Huru wa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Sudan (2009-2010).


Tume ya watu watatu ya Wataalamu wa Haki za Kibinadamu nchini Ethiopia iliundwa na Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa tarehe 17 Desemba 2021 ikiwa na mamlaka ya kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu na ukiukwaji nchini Ethiopia uliofanywa tangu tarehe 3 Novemba 2020 na pande zote kwenye mzozo. Mnamo tarehe 7 Oktoba 2022, Baraza liliamua kuhuisha upya mamlaka ya Tume kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja.


Tume imepangwa kuwasilisha taarifa yake ijayo kwa Baraza la Haki za Kibinadamu wakati wa kikao chake cha kawaida cha 52 (27 Februari-31 Machi 2023).