Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UN wanalaani mashambulizi dhidi ya waathirika wa utumwa wa kisasa na usafirishaji haramu wa binadamu nchini Uingereza

Mwanamke asiye na makazi akiomba pesa katika nji wa London, Uingereza
Unsplash/Tom Parsons
Mwanamke asiye na makazi akiomba pesa katika nji wa London, Uingereza

Wataalamu wa UN wanalaani mashambulizi dhidi ya waathirika wa utumwa wa kisasa na usafirishaji haramu wa binadamu nchini Uingereza

Haki za binadamu

Kuwaandama waathirika wa usafrishaji haramu wa binadamu na aina za utumwa za kisasa kunaondoa huruma ya umma katika hatua za kuwalinda na huenda ikasababisha mashambulizi ya watu wenye itikadi kali dhidi ya makundi hayo, wataalam wa Umoja wa Mataifa wameonya leo, wakiitaka Uingereza kuongeza juhudi za kuwalinda manusura. 

Ukweli wa waathirika wa usafirishaji haramu wa binadamu na aina za utumwa wa kisasa, wakiwemo wahamiaji na raia umeshambuliwa nchini Uingereza, wataalam wamesema kupitia taarifa waliyoitoa hii leo mjini Geneva, Uswisi. 

"Tunasikitishwa na kuongezeka kwa madai ambayo hayajathibitishwa na maafisa wa umma na idara za Serikali kuhusu watu wanaotaka ulinzi chini ya Sheria ya Kisasa ya Utumwa na Utaratibu wa Kitaifa wa Rufaa katika siku na wiki zilizopita. Maafisa wa serikali wametoa madai hayo kwenye vyombo vya habari na tarehe 13 Desemba, Waziri Mkuu Rishi Sunak anaripotiwa kuwa alitoa taarifa ya mdomo kwa Bunge ambapo alisema kwamba "mchujo wa mtu kuchukuliwa kuwa ni mtumwa wa kisasa kitaongezeka kwa kiasi kikubwa". Wameeleza masikitiko yao.  

Vile vile wataalamu wa UN wameendelea kunukuu yaliyoripotiwa kuzungumzwa na Waziri Mkuu wa Uingereza kwamba alisema, "maelezo ya uongo yanayozidisha kiwango cha ulaghai na unyanyasaji katika mfumo wa kuwalinda waathirika wa biashara haramu na utumwa, zinaonesha kuwa walionusurika na vitendo hivi ni wahamiaji katika hali isiyo ya kawaida au wahalifu badala ya kuwa waathirika walio hatarini wa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu" na kwamba wawakilishi wao wa kisheria ni wapenda fursa wasio na akili badala ya watetezi wa haki za binadamu na pia kwamba kuna  

Wataalamu wamebainisha kuwa maombi ya kuthibitisha ushahidi wa mashirika ya kiraia yamepuuzwa mara kadhaa na maafisa husika wa Uingereza. 

Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa walionya kwamba matamshi kama hayo sio tu yanahatarisha ulinzi kwa waathiriwa wa usafirishaji haramu wa binadamu na aina za utumwa wa kisasa bali pia yanaweza kuwatia moyo wasafirishaji haramu wa binadamu. 

"Hii ina athari ya kutisha kwa wale walio tayari kujitokeza kama waathiriwa na wale walio tayari kutoa uwakilishi wa kisheria kwa waathiriwa, na kuzuia juhudi za kuwatambua na kuwalinda waathiriwa na watu walio katika hatari ya usafrishaji haramu wa binadamu na kuwawajibisha wahalifu." Wataalam wa Umoja wa Mataifa wamesema. 

Aidha wataalamu wamewataka viongozi wa umma kujiepusha na kauli za uchochezi na za uongo ambazo zinawanyang’anya uhalali manusura wa utumwa na usafirishaji  haramu ya binadamu na wawakilishi wao wa kisheria.  

Wataalamu hao huru walipendekeza kuwa kama hatua ya awali, serikali iteue mara moja Kamishna Huru mpya wa Kupambana na Utumwa. Nafasi hiyo imekuwa wazi tangu Aprili 2022, licha ya kupewa mamlaka chini ya Sheria ya Utumwa wa Kisasa (2015). 

Wataalamu hao pia wameitaka Serikali ya Uingereza kushughulikia masuala ya haki za binadamu ambayo walikuwa wamebainisha hapo awali kuhusu hatari za usafirishaji haramu wa binadamu na aina za utumwa za kisasa zinazowakabili wafanyakazi nchini Uingereza, wakiwemo wahamiaji na wanaotafuta  

Wataalamu hao wamekuwa wakiwasiliana na Uingereza na Ireland Kaskazini na wanasikitishwa na ukosefu wa majibu kwa mawasiliano yao ya mwisho kuhusu suala hilo na yanayohusiana na hayo.