Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa mwongozo wa utafiti wa magonjwa ya shida ya akili

Dementia ni moja ya sababu kuu za ulemavu na utegemevu miongoni mwa wazee kote ulimwenguni.
WHO/Cathy Greenblat
Dementia ni moja ya sababu kuu za ulemavu na utegemevu miongoni mwa wazee kote ulimwenguni.

WHO yatoa mwongozo wa utafiti wa magonjwa ya shida ya akili

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO hii leo limezindua mwongozo wa kwanza wa kutafiti ugonjwa wa shida ya akili unaoambatana na kushindwa kufikiri na pamoja na kusahau, ikiwa ni njia mojawapo ya kuleta uelewa kuhusu ugonjwa huo, kuzuia na kutibu magonjwa ya msingi ambayo husababisha shida ya akili na wakati huo huo kutoa huduma na msaada kwa watu wenye ugonjwa huo na wale wanaowalea. 

Kwa mujibu wa WHO ugonjwa huo wa kusahau na kushindwa kufikiria  ambao watu wengi huita ni kichaa ni moja ya changamoto kuu za kiafya katika kizazi cha sasa na ni sababu ya saba ya  vifo duniani huku utafiti wa ugonjwa huo ukichukua asilimia 1.5 pekee ya tafiti zote za kiafya. 

Kwa mujibu wa Mwanasayansi Mkuu wa WHO Dkt. Soumya Swaminathan tafiti chache katika eneo hili la afya linarudisha nyuma mpango wa dunia wa afya ya umma wa afya ya akili unaotekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2017 mpaka 2025.

“Kushughulikia shida ya akili kunahitaji kufanyika utafiti na uvumbuzi ili majibu kuweza kupatikana. Zaidi ya yote utafiti wa ugonjwa huu unahitajika kufanywa katika mazingira wezeshi ambapo kuna ushirikiano, uwekezaji na kufikia usawa endelevu.”

WHO imetoa mwongozo huo kwa kuwalenga watunda será, wafadhili, jumuiya za watafiti wa magonja ya shida ya akili iki kuwezesha utafiti kuwa fanisi zaidi, wenye usawa na pale utakapo fanyika kuleta matokeo .

Mwongozo huo umetoa maeneo manne muhimu ya kufanyia utafiti ikiwa ni pamoja na kuangalia uzoefu wa tafiti nyingine za magonjwa ya kuambukiza unaonesha nini, maendeleo ya sayansi na teknolojia bila kusahau akili bandia.

Ashwari, mlezi katika kituo kimoja nchini India akicheka na Didi
WHO/Cathy Greenblat

 

WHO inahamasisha mataifa na taasisi za kimataifa za utafiti pamoja na wafadhili kutumia mwongozo huu katika kufanya maamuzi ya utoaji fedha za kufanya utafiti.

Asasi za kiraia nazo zimehamasishwa kufanya uchechemuzi ili kuhakikisha juhudi za zinaendelea kuhakikisha kuna usawa zaidi kwenye tafiti, zinakuwa shirikishi na zinafanyika kwenye mazingira shirikishi.

“Tunaweza kufikia maendeleo katika utafiti wa ugonjwa wa shida ya akili kwa kuimarisha na kufuatilia vichochezi vya utafiti vilivyoangaziwa katika mwongozo ili ili kusaidia kufanya ni kawaida nzuri utafiti.” Alisema Dkt. Ren Minghui, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa WHO kwenye Magonjwa Yanayoambukiza na Yasiyoambukiza.

WHO imeahidi pia kuendelea kufanya kazi na wadau wote katika sekta husika ili kuhakikisha kwamba hatua zilizoainishwa katika mwongozo huo zinatekelezwa, hatua muhimu zinafikiwa, na malengo ya kimkakati yanatimizwa, kwa lengo kuu la kuboresha ubora wa maisha na msaada unaotolewa kwa watu wanaoishi na shida ya akili. , walezi wao, na familia zao.

Kusoma mwongozo huo bofya hapa