Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wa Ulimwengu, mtakuwa mabadiliko tunayoyasubiri? – Naibu Katibu Mkuu UN 

Naibu Katibu Mkuu Amina Mohammed akihutubia Tamasha la Global Citizen la mwaka 2022 katika Central Park, New York. Tamasha hilo ni tukio la muziki la kila mwaka ambapo mashabiki huchukua hatua za kukomesha umaskini uliokithiri ili kupata kuhudhuria..
UN Photo/Manuel Elías
Naibu Katibu Mkuu Amina Mohammed akihutubia Tamasha la Global Citizen la mwaka 2022 katika Central Park, New York. Tamasha hilo ni tukio la muziki la kila mwaka ambapo mashabiki huchukua hatua za kukomesha umaskini uliokithiri ili kupata kuhudhuria..

Raia wa Ulimwengu, mtakuwa mabadiliko tunayoyasubiri? – Naibu Katibu Mkuu UN 

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed akihutubia umati mkubwa wa watu waliohudhuria ‘Tamasha la Raia wa Ulimwengu’ au Global Citizen Festival, usiku wa kuamkia leo Jumapili katika eneo maarufu kama Central Park jijini New York, Marekani ameuuliza ulimwengu kupitia wakazi wa New York na maelfu wengine waliohudhuria ikiwa wako tayari kuwa mabadiliko chanya ambayo ulimwengu unayasubiri.

Tamasha hili ambalo limefanyika si mbali kutoka yalipo makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambako viongozi wa ulimwengu wanaendelea na Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA77, linadiriwa kuwa lilihudhuriwa na watu Raia wa Ulimwengu, 60, 000 liliendeshwa na mwigizaji, mtayarishaji, mwandishi, na Balozi wa muda mrefu wa tamasha hilo Priyanka Chopra Jonas  ambaye usiku mzima alifanya kazi ya kuwakaribisa jukwaani watu mbalimbali wakiwemo viongozi na waburudishaji mbalimbali kama Mariah Carey na uwepo maalumu wa mwanamuziki Angélique Kidjo kutoka barani Afrika. 

“Habari Wananchi wa Ulimwengu!” Ndivyo alivyoanza kusalimia Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohammed kisha akaendelea kusema, “na ni vizuri kuwa hapa na ninyi nyote. Umati wa ajabu kama nini! Asante kwa kusimama pamoja kama familia moja ya binadamu: matajiri kwa utofauti na sawa katika hadhi zetu.” 

Amina Mohammed mesema ukweli uelezwe kama ulivyo, “Ulimwengu wetu uko katika shida kubwa.” 

Kiongozi huypo wa ngazi za juu katika Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa watu wa ulimwengu wanakabiliwa na janga baada ya janga: Watu wanaumia na “sayari yetu inaungua. Njaa inaongezeka  na tunazidi kutokuwa sawa.” 

Aidha ameeleza kuwa vita inaendelea  na haki za binadamu zinashambuliwa. Lakini akawatia matumaini waliokuwepo akisema, “Hatujakosa tumaini - na si wanyonge!”  

Naibu Katibu Mkuu wa UN vile vile ameweka wazi akisema kila tatizo tunalokabiliana nalo ni tatizo ambalo tumelitengeneza kwa hivyo ni tatizo tunaweza kutatua pamoja. Ulimwengu wa amani unawezekana. Ulimwengu usio na njaa kali unawezekana. Na kuongezeka kwa usawa ni jambo linalowezekana. 

“Ni ulimwengu tuliojiahidi wenyewe, kupitia Ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa na Malengo ya Dunia.” Amesisitiza.  

Naibu Katibu Mkuu Amina Mohammed akihutubia Tamasha la Global Citizen la mwaka 2022 katika Central Park, New York. Tamasha hilo ni tukio la muziki la kila mwaka ambapo mashabiki huchukua hatua za kukomesha umaskini uliokithiri ili kupata kuhudhuria.
UN Photo/Ariana Lindquist
Naibu Katibu Mkuu Amina Mohammed akihutubia Tamasha la Global Citizen la mwaka 2022 katika Central Park, New York. Tamasha hilo ni tukio la muziki la kila mwaka ambapo mashabiki huchukua hatua za kukomesha umaskini uliokithiri ili kupata kuhudhuria.

Lakini wakati unakimbia haraka. 

Akitoa mfano wa Pakistan na janga la tukio la tabianchi, amesema kutakuwa na jingine kesho na ulimwengu una orodha nzito ya Mambo ya Kufanya – “ni Malengo 17 ya Ulimwengu na tunahitaji mikono yenu yote kwenye safu.” 

Akitoa wito kwa umati na kwa ulimwengu amesisitiza akisema, “tunakuhitaji muwawajibishe viongozi wenu, viongozi wangu, na kudai hatua sawa za tabianchi, usawa wa kijinsia, na haki ya kijamii sasa. Sauti zenu ni muhimu. Matendo yako yanahesabika. Badili mafadhaiko yenu kuwa mabadiliko chanya.” 

Lakini mko tayari? 

Aidha Amina Mohammed aliwaeleza hasa vijana waliokuwepo kwamba wanategenewa na wao pia wanaweza kuutegenea Umoja wa Mataifa. Lakini, “Swali langu kwenu ni: Je, mtakuwa mabadiliko tunalosubiri? Je, mtakuwa mabadiliko tunayosubiri?.  Asante, New York!” 

TAGS: Global Citizen Festival, Amina Mohammed, UNGA77