Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa nyingi mbaya kuhusu MONUSCO ni upotoshaji: Bintou Keita

Bintou Keita kutoka Guinea, ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa UN nchini DRC na Mkuu pia wa MONUSCO
N /Eskinder Debebe
Bintou Keita kutoka Guinea, ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa UN nchini DRC na Mkuu pia wa MONUSCO

Taarifa nyingi mbaya kuhusu MONUSCO ni upotoshaji: Bintou Keita

Amani na Usalama

Mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , Bintou Keita amefanya Mkutano na mjadala na wawakilishi wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini humo katika mji mkuu kishasa ili kujadili suala la usalama pamoja na kupambana na usambazaji wa habari za uongo dhidi ya vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa nchini DRC, MONUSCO.

Katika mkutano huo miradi mbalimbali ya MONUSCO pia ilijadiliwa. Akizungumza mbele ya wanazuoni hao wa vyuo vikuu mjini Kinshasa Bintou keita, ameeleza masikitiko yake kutokana na kiwango cha upotoshaji dhidi ya MONUSCO  kupitia mitandao ya kijamii. “Katika mitandao ya kijamii, kile ninachokiona mara nyingi, ninashangazwa na kiwango cha upotoshaji, upotoshaji wa habari na kiwango cha hila kilichopo ili kulichafua jina la Monusco. ninachotaka tu kusema ni kwamba katika kile tunachokiona mashambulizi ya hivi karibuni unajua sisi pia tuna taarifa tunajua kwamba kuna watu ambao wamelipwa na wanaendelea kufanya kila liwezekanalo  ili watu waendelee kushambulia moja kwa moja vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini DRC Monusco”. 

Aidha Bi Keita ameongeza kuwa vikosi vya MONUSCO kwa wakati wote si tu vimefanya kazi kubwa ya kuunganisha na kuweka amani katika sehemu kubwa ya DRCl akini pia imekuwa na miradi mbalimbali ya maendeleo. 

“Kazi nyingine ni utulivu na hii ni miradi tuliyonayo ndani ya jamii na hii ni miradi ya haraka haraka. wengi mliotoka Beni kwa sasa mwanga uko katika barabara za jiji la Beni, nani aliweka taa za sola? ni MONUSCO. nani anatengeneza madaraja ili barabara ziwe nyingi zaidi ? ni wahandisi raia kutoka MONUSCO au wahandisi wa kijeshi kutoka kikosi hicho. Mambo mengi unaona viwanja vya ndege ambavyo pia vinatumika leo kwa ndege za taifa la Congo kutua vilitengenezwa na monusco. Uwanja wa ndege wa Goma, ambao sasa umekuwa wa kimataifa, mwanzoni hakukuwa na kitu, ilikuwa shukrani kwa Monusco”. 

Askari mwanamke kutoka Afrika Kusini akiwa doriani huko DRC
MONUSCO
Askari mwanamke kutoka Afrika Kusini akiwa doriani huko DRC

Baada ya maelezo yake ya takriban dakika arobaini na tano, ukawadia wakati wa wanavyuo kuuliza maswali na kupokea majibu yake. 

Hata hivyo baadhi ya wanazuuoni walionyesha mitizamo yao kuusu mkutano huoo miongoni mwao ni Emeraude Balenda mwanafunzi wa chou kikuu Kinshasa “Mimi ntasema kuwa sio kwa Munusco ya kushambuliwa maana tunawajibika sote kuleta amani.kuna jukumu letu binafsi,la serekali na Monusco pia ambayo ni moja ya washirika wa nchini yetu DRC.Shida yetu sisi nikwamba tunataka kuona amani “ 

 Naye Ravallely Ntumba Kudinga mwanafunzi wa chuo kikuu cha IFASIC Kinshasa amesema “ Ilikuwa ni fursa kwangu kwa sababu tulipata taarifa nyingi kutoka mtaani kuhusu munusco jambo ambalo si la kweli hivyo kubadilishana mawazo na Bintou Keita imetupa mtazamo mwingine wa Monusco. Zamani tufikiria kwamba Monusco ipo kwa ajili ya kupata pesa tu. haijalishi kama kutauwa na amani au la, lakini pia tunaelewa kwamba ni wasiwasi wa kila mtu anayefanya kazi huko Monusco kurejesha amani”. 

 Hata hivyo bwana Theodore Kanyama Mwanafunzi katika chuo kikuu cha UPN Kinshasa anasema kuwa serekali inalo jukumu la kuhamasisha raia ili waelewe umuhimu wa Vikosi vya Monusco nchini DRC.  “Nadhani kwamba majukumu yanategemeana kama Bibi Bintou Keita alivyosema, kuna kinachohusiana na mawasiliano, serikali inapaswa kufanya kila iwezalo kuwaeleza wananchi nini dhamira ya monusco katika ardhi yetu. ieleze kwa uwazi malengo ya monusco. pia kuna ambacho ningeomba kama pendekezo kwa serikali yetu ni kuimarisha jeshi letu maana tukiwa na jeshi imara MONUSCO haitaingilia kati . ikiwa Monusco inaingilia kati kulinda amani ni kwa sababu jeshi letu linashindwa”. 

Katika hali ya utulivu na ustaraabu, mkutano huo ulihuzuriwa na zaidi ya wanafunzi 500 kutoka viuo vikuu mbalimbali vya mji wa Kinshasa.