MONUSCO yajenga uwezo polisi kuelekea uchaguzi mkuu DRC

13 Disemba 2017

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO unaendesha mafunzo ya kujengea uwezo wasimamizi wa uchaguzi pamoja na polisi nchini humo wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.

Mkuu wa kitengo cha polisi, MONUSCO Kamishna Mkuu Awalé Abdounasir, amesema mafunzo hayo yanayofanyika kwenye mji mkuu Kinshasa, yanalenga kuhakikisha polisi wanazingatia sheria na kanuni wakati wa kipindi cha uchaguzi.

Naye Rais wa tume ya taifa ya uchaguzi, CENI, Corneille Nanga, akatumia semina hiyo elimisha kuhusu sheria ya uchaguzi na mchakato wa uchaguzi nchini DRC.

Mafunzo hayo ya siku tano yanajumuisha washiriki 100 wakiwemo wakaguzi wa uchaguzi, maafisa wa polisi na yatamalizika Ijumaa.

Uchaguzi wa rais, wabunge na magavana wa majimbo nchini DRC utafanyika tarehe 23 mwezi disemba mwakani 2018.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter