Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukanda wa Karibea ni kitovu cha janga la tabianchi duniani- Guterres

Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akiwa kwenye ndege akitazama eneo la hifadhi la Suriname lenye ukubwa wa ekari milioni 1.6 za msitu mnene wa kitropiki.Eneo hilo liko katika ukanda wa msitu mnene wa Amazon.
UN News/Evan Schneider
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akiwa kwenye ndege akitazama eneo la hifadhi la Suriname lenye ukubwa wa ekari milioni 1.6 za msitu mnene wa kitropiki.Eneo hilo liko katika ukanda wa msitu mnene wa Amazon.

Ukanda wa Karibea ni kitovu cha janga la tabianchi duniani- Guterres

Tabianchi na mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye ametamatisha ziara yake huko Suriname hii leo kwa kupata ziara ya angani ya msitu mnene wa Amazon, iliyomwezesha kuona uzuri wa eneo hilo na papo hapo hatari za kutoweka ambazo msitu huo wa mnene wa mvua kutokana na ukataji holela wa miti.

 

Paramaribo ni mji mkuu wa Suriname katika ukingo wa mto Suriname. Picha hii kutoka angani ni wakati Katibu Mkuu wa UN akisafiri kwa ndege kutoka mjini kwenda kupata taswira ya angani ya Msitu mnene wa Amazon 3 Julai 2022
UN News/Laura Quinones
Paramaribo ni mji mkuu wa Suriname katika ukingo wa mto Suriname. Picha hii kutoka angani ni wakati Katibu Mkuu wa UN akisafiri kwa ndege kutoka mjini kwenda kupata taswira ya angani ya Msitu mnene wa Amazon 3 Julai 2022

Siku ya mwisho ilianza kwa kupanda ndege ndogo iliyochukua muda wa dakika 90 hadi kwenye ukumbi wa mkutano wa Jumuiya ya soko la pamoja la nchi za ukanda wa Karibea, CARICOM.

Akiwa angani kupitia eneo hilo la hifadhi la maliasili la Suriname lililotangazwa na UNESCO kuwa eneo la urithi wa dunia, akitokea mji mkuu Paramaribo, Katibu Mkuu aliona kutoka angani ukijani uliosheheni na maua ya rangi mbalimbali sambamba na mto Coppename na mito mingine midogo kama mto Lucie, Saramacca ikipita katikati ya miti kama vile michoro ya mandhari.

Hata hivyo kabla ya kufika eneo hio la hifadhi, Guterres alijionea jinsi misitu ya Suriname inavyotishiwa na shughuli za uchimbaji madini na uzalishaji wa mbao vyote vikichochewa na ili kukuza uchumi. Akiwa angani ameona maeneo ya misitu yaliyo wazi na majitaka kutoka kwenye uchenguaji wa madini yakimiminikia mitoni.

Zama za nyakati za hatari kubwa

Ijapokuwa Suriname ni sehemu ya bara la Amerika ya Kusini, inatambuliwa kuwa taifa la Karibea kutokana na historia yake, utamaduni na changamoto zingine zinazokabili mataifa ya visiwa vidogo.

Hatimaye ndege ilitua kwenye mji mkuu Parimaribo na kisha Katibu Mkuu akaingia kwenye ukumbi wa mkutano waw a 43 wa nchi wanachama wa CARICOM.

Hapo amegusia hatua ongozi ya ukanda huo katika kuchukua hatua dhidi ya tabianchi na jinsi wanaishi pamoja na utofauti wao.
Amegusia pia hatua zinazochukuliwa na ukanda huo wakati huu sayari na dunia inakabiliwa na janga la tabianchi sambamba na COVID-19 na changamoto za kifedha zinazokumba dunia.

Eneo la kati la hifadhi la Suriname lina ukubwa wa ekta milioni 1.6 za msitu wa kitropiki na linahifadhi kingo za maji za mto Coppername. eneo hilo linatambuliwa na UNESCO kuwa urithi wa dunia.
UN News/Laura Quinones
Eneo la kati la hifadhi la Suriname lina ukubwa wa ekta milioni 1.6 za msitu wa kitropiki na linahifadhi kingo za maji za mto Coppername. eneo hilo linatambuliwa na UNESCO kuwa urithi wa dunia.

“Utajiri wa utofauti, kuunganisha ardhi na bahari na kulinda mifumo anuai ya pwani iliyo hatarini kutoweka, sambamba na mikoko ni mambo sahihi kabisa na alama ya mataifa ya Karibea- yakikabiliana na changamoto, yakidaka furs ana kulinda zawadi za asili,” amesema Katibu Mkuu akihutubia wakuu wa nchi wanachama wa CARICOM akichochea na ziara ya kutia moyo huko Paramaribo aliyofanya jumamosi kuona jinsi taifa hilo linapambamba na kukabili hewa ukaa maeneo ya pwani,

Bwana Guterres ametambua kuwa nchi za visiwa vidogo ambavyo fukwe zake ziko ukanda wa chini katika ukanda a Karibea, ziko hatarini zaidi kwenye kile anachokiita, “changamoto kubwa zaidi inayokabili dunia hivi sasa,” — janga la tabianchi.
 
“Ukanda wa Karibea ni eneo la hatari zaidi au lilicho kwenye ukanda wa chini zaidi kwa janga la sasa la tabianchi,” amesema Katibu Mkuu akisisitiza, “kwa bahati mbaya hilo si janga pekee ambalo ukanda huu unakabiliana nalo.”
 
Mkutano wa mwaka huu wa CARICOM unakuja wakati tuko katika hatari ya juu zaidi kwa watu na sayari yao, akigusia madhara ya janga la COVID-19 katika mifumo ya afya na utalii pamoja na ukuaji wa uchumi, uwekezaji wa kigeni ambavyo sasa vinachochewa zaidi na vita ya Ukraine.

Majawabu ya kijasiri

Katika Mkuu amewaeleza viongozi wa CARICOM kuwa majawabu ya kijasiri ni muhimu katika kushughulikia changamoto za sasa akitaja maeneo matatu

1. Hatua za tabianchi ziendane na kiwango cha janga lenyewe 

Katibu Mkuu ametaka hatua za dharura za kupunguza kiwango cha joto duniani ili kisizidi nyuzijoto 1.5 katika kipimo cha selsiyasi (1.5C), usaidizi katika mikakati ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, msaada wa fedha ili hatimaye nchi na jamii ziwe na mnepo.
“Nashukuru viongozi wa Karibea kwa kusaidia kuonesha njia. Navutiwa na juhudi zenu nyingi za kulinda baiyonuai na zawadi za kiasili ikiwemo juhudi kutoka jamii za watu wa asili,” amesema Katibu Mkuu.
 
Ameongeza kuwa hatua Zaidi zinahitajika kuchukuliwa na watu wote, lakini Zaidi ni kundi la nchi 20 au G20, ambazo zinachangia asilimia 80 ya hewa chafuzi duniani.
 
Amesisitiza kuwa nchi Tajiri zinahitaji kuonesha njia katika njia sawia hususan mapinduzi ya nishati jadidifu na “zinapaswa kutimiza ahadi zao za kuchangia dola bilioni 100 kufadhili miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi kuanzia mwaka huu.

2. Marekebisho ya mfumo wa fedha duniani uliomomonyoka kimaadili

Katibu Mkuu amesisitiza kuwa uchumi wa nchi zinazoendelea unahitaji msaada wa fedha bila gharama au kwa gharama ndogo, sambamba na madeni yao wapatiwe unafuu na yaangaliwe upya.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  António Guterres akihutubia mkutano wa kawaida wa 43 wa jumuiya ya nchi za Karibea, CARICOM huko Paramaribo, mji mkuu wa Suriname.
UN /Evan Schneider
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia mkutano wa kawaida wa 43 wa jumuiya ya nchi za Karibea, CARICOM huko Paramaribo, mji mkuu wa Suriname.

“Kuhusu madeni, tunahitaji unafuu wa haraka kwa nchi zinazoendelea ambazo deni lao karibu litapitiliza,” amesema Katibu Mkuu.
 
Amesema anaunga mkono kuanzishwa kwa Mfuko wa Mnepo kwa nchi za Karibea na mrekebisho ya mfumo wa kimataifa wa fehda ili kusaidia ukanda huo kuchukua hatua bora Zaidi na kuzuia kutumbukia kwenye hatari kutokana na hali zinazotokea nje ya ukanda huo.
 
“Ni dhahiri mifumo  yetu ya zamani imetuangusha, ni wakazi wa kubadilisha,” amesema Guterres akipendekeza marekebisho Zaidi ya muundo wa kifedha wa kuangalia pato la mtu na badala yake kuwa na mfumo wenye vigezo vingi vya kuamua jinsi ya kutoa msaada wa fedha

3. Kuendeleza vita dhidi ya COVID-19

Hatimaye Katibu Mkuu ametaka serikali, mashirika na kampuni za dawa kushirikiana ili vipimo, vitendanishi, tib ana chanjo viweze kutengenezwa ndani ya nchi badala kuagizwa kutoka nje.

“Bado tuko ndani ya kiza kinene, na tunahitaji kuendelea kushirikiana kukomesha kusambaa kwa virusi kwenye ukanda wa Karibea, na tufanye hivyo kwa kuweka hatua za afya ya umma zilizothibitishwa na kujiandaa kwa majanga yajayo ya kiafya kupitia uwekezaji thabiti kwenye kujiandaa na pia mafunzo,” amesema Guterres akiongeza kuwa nchi katu zisiwe hazijajiandaa.
 
Ametamatisha kwa kusisitiza kuwa Umoja wa Mataifa umesimama kidete na kusaidia nchi za Karibea katika kufanikisha majawabu hayo.