Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunaitunza misitu ya Amazon kwa kuwa inatutunza-Watu wa asili

Msitu wa Amazon
UN
Msitu wa Amazon

Tunaitunza misitu ya Amazon kwa kuwa inatutunza-Watu wa asili

Tabianchi na mazingira

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP linafanya kazi kwa kushirikiana na serikali ya Peru na wananchi wanaofuatilia mazingira ili kutafuta mbinu za kuyarekebisha maeneo ambayo yamaethiriwa na uchimbaji wa mafuta katika msitu wa Amazon

Ndani ya msitu wa Amazon, nchini Peru, watu wa jamii ya asili ya Loreto Peru, wanaelewa thamani ya msitu huu na rasilimali zake. 
 
Kwa zaidi ya miaka 10 wamekuwa wasimamizi wa kufuatilia na kutoa tarifa kuhusu matokeo ya uchimbaji mafuta katika eneo hilo.
 
Marcial Sánchez, mfuatiliaji wa mazingira wa jamii ya watu wa Quechua  anaeleza,  “Msitu wa Amazon una eneo kubwa . Eneo hilo linamaanisha maisha watu wote wa Peru, kwa ulimwengu mzima. Dunia ni kama baba na mama ambao wanaokulisha kila siku. Inakupa chakula. Inakupa afya. Inakupa uzima. Kama huna fedha, unachukua ndoano yako na kuleta kilo mbili au tatu za samaki. Na kupata mimea na yucca kutoka nchi yako, na kufanya chakula na familia”
 
Marcial Sánchez, anasema kama wafuatiliaji wa mazingira, tunalifuatilia eneo hili, tukipata  eneo ambalo limeathirika wanakusanya Ushahidi. 
 
Naye Dugner Tapuy, mwangalizi wa mazingira kutoka jamii ya watu wa Quechua anasema huwa wanarekodi pia video ya dakika moja au mbili. Wanatafuta eneo kupitia teknolojia ya GPS na kwamba huo ni wajibu wao kama watu wa asili kuhakikisha wanaheshimu mazingira na kipengele cha jamii yao.
 
Marcial Sánchez, wa jamii ya asili ya Quechua anarejea tena na kueleza mafanikio ya zoezi lao, “Ninaamini ripoti zetu, picha zetu, ushahidi ambao tunatuma umekuwa wa faida kwasababu kupitia taarifa hizo, kumekuwa na mashirika mengi yanayoonekana hapa. Hata Umoja wa Mataifa ambao hautukuwahi hata kuuona katika ndoto zetu au kukutana nao, sasa wako hapa. Ni juhudi za kaka na dada wa hapa. Tunayafanya haya kwa mapenzi tuliyo nayo kwa watu wa hapa. Ni kuwalinda watoto wetu, kaka na dada zetu ambao wako hapa. Siyo kwa ajili yangu au Andoas, lakini dunia ni kwa ajili ya watu wote”


Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa, tafadhali jisajili na pia unaweza kupakua apu ili kuweza kusikiliza wakati wowote popote ulipo.