Zaidi ya wahamiaji 1000 kutoka Afrika Mashariki wamekufa au kutoweka

18 Mei 2022

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema zaidi ya wahamiaji 1,000 wamefariki dunia au kutoweka tangu mwaka 2014 walipokuwa wakijaribu kuondoka Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika. 

Taarifa iliyotolewa na IOM kutoka Geneva Uswisi imesema wengi wa wahamiaji hao walikuwa wakisafiri kutoka Pembe ya Afrika hadi Rasi ya Uarabuni au kutoka Pembe ya Afrika kwenda Afrika Kusini.

Shirika hilo limeeleza kuwa wahamiaji wanakabiliwa na hatari kama vile usafiri wa hatari, kukosa hewa safi, vurugu, kuachwa na walanguzi wanaoahidi kuwasafirisha, ufikiaji mdogo wa huduma za matibabu na kuwekwa kizuizini.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter