Uchumi wa dunia kupungua kwa asilimia 3.1: UN

Idara ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya Uchumi na Kijamii imetoa utabiri unao onesha kupungua kwa ukuaji wa uchumi wa dunia hadi asilimia 3.1 kwa mwaka 2022, kutoka asilimia 4.0 iliyo tabiriwa mapema mwezi Januari (2022).
Ripoti ya Hali ya Kiuchumi Duniani na Matarajio yake kwa nusu mwaka wa 2022 imetolewa leo jijini New York Marekani na imeeleza sababu kubwa za kupungua kwa ukuaji wa uchumi duniani kuwa ni pamoja ya vita inayoendelea nchini Ukraine na janga la COVID-19 ambavyo kwa pamoja zimezidisha kupanda kwa bei za bidhaa na kuongeza mfumuko wa bei duniani kote.
Mbali na uchumi wa dunia kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na vita nchini Ukraine, kuibuka kwa awamu mbalimbali za mawimbi ya janga la COVID-19 kumefanya hali ya kupata fedha kuwa ngumu zaidi ya ilivyotarajiwa hususan katika nchi zinazoendelea.
Ripoti hiyo imeeleza nchi zinazoendelea ingawa hali ni mbaya lakini pato linatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 4.1 kwa mwaka 2022, hata hivyo kupanda kwa mfumuko wa bei na ukuaji taratibu kwa polepole kwa nchi za Marekani, China na Umoja wa Ulaya kunatarajiwa kuongeza gharama za kukopa za nchi zinazoendelea na kuzidisha mapengo ya ufadhili.
“Hali ngumu za kifedha za nje zitaathiri vibaya matarajio ya ukuaji wa uchumi hususan kwa nchi zinazotegemea zaidi masoko ya mitaji ya kimataifa, hali hiyo itachangia kuongezeka kwa uhaba wa chakula, hasa barani Afrika.”
Nchi zinapaswa kufanya?
Pia nchi zitahitaji kufanya marekebisho ya kina ya deni na msamaha wa deni kwa nchi maskini, hasa nchi masikini zaidi.
Kusoma ripoti kamili bofya hapa.