Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Kakuma, Kenya - 26 Machi, 2018: Wagonjwa wakiwa katika Duka la Dawa la Hospitali ya Misheni ya Kakuma. Hospitali hii ya Kaskazini mwa Kenya ni mojawapo ya vituo vichache katika eneo la Turkana ambapo wagonjwa wanaweza kupata ushauri wa ophthalmologic na u

Nilitamani kuwa muuguzi tangu ningali mdogo

WHO/Sebastian Liste through NOOR
Kakuma, Kenya - 26 Machi, 2018: Wagonjwa wakiwa katika Duka la Dawa la Hospitali ya Misheni ya Kakuma. Hospitali hii ya Kaskazini mwa Kenya ni mojawapo ya vituo vichache katika eneo la Turkana ambapo wagonjwa wanaweza kupata ushauri wa ophthalmologic na upasuaji

Nilitamani kuwa muuguzi tangu ningali mdogo

Afya

Muuguzi Rebecca Deng ambaye ni mkimbizi wa Sudan Kusini anayeishi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya ameisihi jamii kuhakikisha inapata elimu sahihi ya afya ya uzazi pamoja na kuhimiza wanawake na wasichana kutoacha kujiendeleza kielimu. 

“Wakati nakua nilipenda kusema Lazima nifanye kazi hospitalini,” ndio inavyoanza video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UNHCR ikimuonesha Rebecca Deng ambaye ni muuguzi wa kujitolea wa shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya. 

Deng ni mkimbizi wa Sudani Kusini anayeishi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko nchini Kenya ambaye kupitia programu ya Uzazi salama inayofadhiliwa na UNHCR amekuwa akitoa elimu kwa wakimbizi wenzake kambini hapo. 

Anasema “ Nina furaha sana kuwasaidia watu, Jamii ilizoea kuniita iwapo kulikuwa na mjamzito aliyetaka kujifungua, walikuwa wanakuja kugonga mlango wangu nami nilivaa aproni yangu na kwenda mara moja.” 
Muuguzi huyu anaeleza jukumu lake hasa ni kuelimisha jamii na kuwaonesha faida za kwenda kujifungulia hospitalini. 

Anasema “ Unapojifungulia hospitalini hata kama tatizo linajitokeza daktari anaweza kulitatua. Na pia tunawaonesha jinsi ya kutunza ujauzito, kwa kuwa ukifuata vyema huduma za ujauzito daktari anaweza kuchukua vipimo vingi vya damu na kuweza kukuhudumia.” 

Pamoja na kuwapatia elimu, wajawazito pia wanapewa namba ya simu ya gari la wagonjwa iwapo watakuwa na dharura au wamepata uchungu ili waweze kupiga gari liwafuate kuwapeleka hospitali. 

Pichani iliyopigwa kutoka angani inaonyesha sehemu ya makazi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya
Picha/Siegfried Modola
Pichani iliyopigwa kutoka angani inaonyesha sehemu ya makazi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya

Lakini huduma hii muhimu ilisitishwa  kipindi cha janga la coronavirus">COVID-19, hawakuweza kutoa elimu na hali ilikuwa mbaya, wasichana wengi walipata ujauzito na hapa anatoa ushauri kwa wasichana. 

Anasema “ Ushauri wangu kwa wasichana kwanza waendelee na masomo, pili tunazungumza nao kuhusu ndoa katika umri mdogo. Tunasema waachwe kwanza waendelee na masomo. ...... Hata mimi mpaka sasa hivi naendelea na masomo .. Jioni najifunza lugha ya Kiingereza katika makazi ya wakimbizi.” 

Na mwisho ana ushauri kwa wanawake wote ... “ Tuendelee kuwaelimisha wanawake wajiendeleze kielimu, hakuna tofauti kati ya wanaume na wanawake, kazi inayofanywa na wanaume inaweza pia kufanywa na wasichana na wanawake.”