Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York kuzima taa zake leo usiku

Mwaka 2018, Umoja wa Mataifa uliungana na wengine duniani kote kuzima taa katika Makao yake Makuu na maeneo mengine ili kuadhimisha “saa ya sayari dunia”
UN Photo/Evan Schneider
Mwaka 2018, Umoja wa Mataifa uliungana na wengine duniani kote kuzima taa katika Makao yake Makuu na maeneo mengine ili kuadhimisha “saa ya sayari dunia”

Jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York kuzima taa zake leo usiku

Masuala ya UM

Leo Jumamosi, tarehe 26 Machi 2022, Umoja wa Mataifa utashiriki tena katika "Saa ya Dunia", mpango wa kimataifa unaounganisha mamia ya mamilioni ya watu binafsi, makampuni, mashirika na serikali duniani kote kuzima taa zao kuanzia saa mbili na nusu usiku (2:30 usiku) hadi Saa tatu na nusu usiku 93:30 usiku) ili kuzingatia masuluhisho ya watu katika kulinda sayari na kujenga mustakabali mzuri na endelevu. 

Mwaka jana 2021 katika maadhimisho kama haya, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress alibainisha kwamba uharibifu wa tabianchi, upotevu wa baionuai na uchafuzi wa mazingira unatishia maisha, kazi na afya duniani kote na kwa hivyo ni muhimu "kuweka amani na asili." 

"Bila msaada wa asili, hatuwezi kustawi au hata kuishi katika sayari hii ya Dunia", Katibu Mkuu Guterres alisisitiza katika siku hii ambayo huadhimishwa kila mwaka Jumamosi ya mwisho ya mwezi Machi.