Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila kuishi kwa amani na mazingira asilia hatma yetu ni mtihani:Guterres

Mwaka jana, Umoja wa Mataifa uliungana na wengine duniani kote kuzima taa katika Makao yake Makuu na maeneo mengine ili kuadhimisha “saa ya sayari dunia”
UN Photo/Evan Schneider
Mwaka jana, Umoja wa Mataifa uliungana na wengine duniani kote kuzima taa katika Makao yake Makuu na maeneo mengine ili kuadhimisha “saa ya sayari dunia”

Bila kuishi kwa amani na mazingira asilia hatma yetu ni mtihani:Guterres

Tabianchi na mazingira

Katubu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema dunia inahitaji kuwa na amani mazingira asili kwani bila msaada wa mazingira asilia hakuna uhai na hakuna maisha katika sayari hii.

Guteerres ameyasema hayo kupitia ujumbe wake maalum kwa ajili ya “Saa ya sayari dunia” inayoazimishwa leo na kuongeza kuwa changamoto zinazoletwa na mabadiliko ya tabianchi, kupotea kwa bayoanuai na uchafuzi wa mazingira vinatishia maisha, ajira na afya.
Na kwa mantiki hiyo amesisitiza kwamba “ni wakati wa kutafakari upya na kubadili uhusiano wetu na maumbile asilia. Mwaka 2021 ni mwaka wa kubadili mwelekeo. Suluhu zipo, za gharama nafuu, zinazowezekana na za kuaminia.”
Katibu Mkuu ameongeza kuwa dunia inaweza kuza;lisha nishatyi jadidifu na kuwa na mifumo endelevu ya chakula kwa wote.
Kwani “Tunawexza kupunguza gesi chafuzi na kutumia suluhu za kiasili zinazoweza kutusaidia kujenga dunia yenye mnepo zaidi na isiyo na hewa chafuzi.Stote tunapaswa kutimiza wajibu wetu ili kulinda sayari yetu.”

Amehitimisha ujumbe wake kwa kusema kuwa Umoja wa Mataifa unajivunia kujumuika katika juhudi za kimataifa kuadhimisha saa ya sayari dunia kwani ni kumbusho kwamba hatua zozote hata kama ni ndogo zinaleta mabadiliko makubwa. 

“Kwa hivyo, jiunge nami na watu kila mahali kwa kuzima taa zenu kwa saa moja leo Jumamosi Machi 27 saa 2:30 usiku, saa za mahali ulipo. Katika mwaka huu wa changamoto nyingi acha matendo na sauti zako zitume ujumbe bayana kwa viongozi kila mahali kwamba sasa ni wakati wa kuwa jasiri na mwenye tamaa. Hebu na tuuonyeshe ulimwengu kwamba tumeamua kulinda nyumba pekee ambayo sisi wote tunaitumia.”