Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Visiwa vya Marshall vyajizatiti kupambana na janga la Corona 

Wakazi wa visiwa vya Marshall
IOM Video Screenshot
Wakazi wa visiwa vya Marshall

Visiwa vya Marshall vyajizatiti kupambana na janga la Corona 

Afya

Je unafahamu kuna nchi chache duniani ambazo mpaka sasa zimefanikiwa kujilinda na hazijapata hata mgonjwa mmoja wa Corona?. Moja ya nchi hizo ni Jamhuri ya visiwa vya Marshall. 

Jamhuri ya visiwa vya Marshall au kwa jina lingine RMI ni nchi yenye ukubwa wa kilometa za mraba 181 ikikaliwa na watu 54,000, na ni niongoni mwa nchi chache duniani ambazo hazijapa mgonjwa hata mmoja wa Corona au COVID-19.

Lakini kwa kuwa wananchi wa nchi hii wanazunguka na kusafiri nchi za Jirani kama Ufilipino, Papau new Guinea na Indonesia ni dhahiri wanahitaji kujilinda na kujiandaa na janga hili la dunia ndio maana benki ya dunia imetoa msaada wa dola Milioni 2.5 kwa ajili ya vifaa vya kufanyia uchunguzi wa watu wanaoingia na kutoka katika visiwani pamoja na vifaa tiba katika hospitali zao.

Francyne Wase- Jacklick ni mkurugenzi katika wizara ya afya na huduma za watu.

“RMI tumepata bahati sana kupokea msaada huu wa kusaidia mpango wa kushughulika na janga la COVID-19. Kupitia fedha hizi, tumeweza kufanya vitu kama mafunzo kwa wauguzi, na kununua vifaa vya kupimia watu.”

Lilieta Snoddy ni Kaimu mkuu wa wauguzi katika hospitali ya Ebeye anasema kwa miaka 19 aliyofanya kazi hajawahi kuona msaada mkubwa kama huu.

“Tunashukuru kwa msaada huu, tumepokea machine za kuweza kufuatilia hali ya mgonjwa, machine za kusaidia upumuaji, Exray ndogo, nguo maalum za kuvaa wakati tunawatibu wagonjwa wa Corona, vitu ambavyo wakati janga hili linaanza hatukuwahi kuwaza kama tutakuwa navyo hususan mashine za kupumuliwa, sasa kila kitanda kina mashine yakumsaidia mgonjwa kupumuwa, na nafikiri huu ni msaada mkubwa”

Benki ya dunia inatoa msaada wa haraka katika sekta ya afya kwa nchi zaidi ya 100 duniani hasa zile masikini na ambazo wananchi wake wapo hatarini zaidi kupata maambukizi.