Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kama ng’ombe wangekuwa nchi, nchi hiyo ingekuwa ya tatu kwa uchafuzi wa mazingira duniani.

Burger pamoja na viazi
Public domain
Burger pamoja na viazi

Kama ng’ombe wangekuwa nchi, nchi hiyo ingekuwa ya tatu kwa uchafuzi wa mazingira duniani.

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Pengine si wengi wanaoiingia katika mghahawa unaouza mathalani burger yaani nyama iliyofunikwa kwa mkate, wanaowaza kuwa chakula hicho wanachokinunua ni sawa na kushiriki katika kuharibu mazingira. Harakati za binadamu katika kutengeneza nyama ni njia mojawapo za uharibifu unaoacha alama duniani.

Kile kinachokuwa katika mawazo yetu ni nyama na jibini, pengine sasa ni wakati wa kuanza kuwaza kubadili fikria na kugeukia mazingira.

Hekta nyingi za misitu ya asili huko Amerika ya kusini zinakatwa kwa ajili ya kuandaa malisho ya ng’ombe ili hatimaye kipatikane chakula kinachopendwa cha mwanadamu, burger na nyama. Utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo , FAO unaonesha kuwa asilimia moja ya karibu robo kilo ya nyama inayotengeneza bager inakuwa imenyonya karibia lita 1,695 za maji kulingana na kule ilikotengenezwa.

Na uhitaji wa nyama kwa mwanadamu unazidi kuongezeka. Miaka ijayo nyama italiwa zaidi kwa kiwango kikubwa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya mwanadamu. FAO linakadiria kutakuwa na ongezeko la asilimia 76 katika matumizi ya nyama kufikia mwaka 2050.

Kundi la ng'ombe malishoni karibu na kijiji huko Kazakhstan
Daniil Nenashev/World Bank
Kundi la ng'ombe malishoni karibu na kijiji huko Kazakhstan

 

Kuhusu gharama zilizofichika, ambazo wanadamu wanaweza kukumbana nazo, afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP James Lomax anasema, “Tunahitaji kuwa wakweli. Kuondoa kabisa nyama katika mlo wa watu wengi siyo chaguo lao. Mazao yanayotokana na ufugaji ni muhimu kwa chanzo cha vitamini na protini na pia chanzo cha mapato kwa watu wengi maskini duniani.Na ufugaji mdogo una tofauti sana katika mazingira ukilinganisha na ule wa kiviwanda”

Kuanzia mifumo ya ufugaji ile ya barani Afrika na Amerika ya kusini hadi ile ya kwa ajili ya viwanda barani Ulaya na Amerika Kaskazini, kila mfumo una faida na hasara, ameongeza afisa huyo wa UNEP.

“Lakini kwenye kiini cha suala la mazingira ni namna nyama inavyozalishwa na hasa jinsi inavyotumika. Kupunguza ulaji wa nyama za Wanyama waliofugwa ni jambo jema kwa binadamu na dunia.”

Ufugaji mzuri wa ng'ombe ni moja  ya miradi inayokomboa wakazi kwenye nchi ambazo zimewekeza vizuri katika sekta hiyo
Patrick Zachmann/Magnum Photos for FAO
Ufugaji mzuri wa ng'ombe ni moja ya miradi inayokomboa wakazi kwenye nchi ambazo zimewekeza vizuri katika sekta hiyo

 

Uhitaji mkubwa wa nyama una madhara mengine ambayo ni gharama kwa binadamu, gharama ambayo inaweza isiwe inaonekana kwa wazi haraka. Kilimo kinatumia maji safi kuliko shughuli nyingine ya binadamu. Wakati kuwafuga Wanyama inachukua hadi asilimia 80 ya ardhi ya kilimo, ufugaji unachangia asilimia 18 ya calories duniani.

Chakula kwa ajili ya mifugo kilichotengenezwa kutokana na soya, moja ya bidhaa kubwa zinazosafirishwa kutoka Amerika ya kusini, kinaaongoza kwa ukataji mkubwa wa miti na kuwaondoa wakulima na wakazi wa asili katika maenewo yao duniani kote.

Ni vigumu sana kugundua jinsi chakula cha binadamu ikiwa ni pamoja na matumizi ya nyama kinavyochangia kifo au ugonjwa, kwa sababu ya mambo mengine mengi yanayohusika. Hata hivyo inafahamika kwamba kula nyama kwa kiwango cha ziada kuna athari mbaya kwa afya ya binadamu.

Dawa zinazotumika kukuzia mifugo na zile za kuwakinga na magonjwa, mara nyingi huishia kuingia katika vyakula na hivyo kuchangia dawa za matibabu kwa binadamu kuwa na usugu. Imeelezwa hivi karibuni pia kuwa maduka ya kuuza vyakulahutumia nyama zilizo na dawa kama antibaiyotiki.

Nyama ikiwa katika soko la Hamarwayne, Mogadishu Somalia.
AMISOM/Omar Abdisalan
Nyama ikiwa katika soko la Hamarwayne, Mogadishu Somalia.

Ni nini kifanyike?

UNEP inasema inabidi tule kiasi kidogo cha nyama au hata kula nyama nyeupe mathalani ya kuku ambayo inaweza kuwa Rafiki kwa mazingira kuliko nyama nyekundu mfano ile ya ng’ombe.

Watengenezaji wa vyakula ambavyo vinaelekea kuwa kama nyama lakini kimsingi vinatumia mimea, wanasema bidhaa zina kiasi kidogo cha mafuta na lehemu kuliko vyakula vyao vilivyotengenezwa kwa nyama. Kuna mtindo mpya ambao bado uko kwa kiasi kidogo lakini unakua, ‘Nyama’ isiyo na nyama.

Utafiti unaonesha kuwa mmarekani anakula angalau burger tatu kwa wiki. Ikiwa kila moja ya Burger ingebadilishwa na kuwa burger mbadala za ‘Beyond Meat’ zisizotumia nyama lakini zimetengenezwa kwa namna ya kuelekea kufanana na nyama, hiyo ingekuwa sawa na kuondoa barabarani magari milioni 12 yanayochafua hewa.