Ni wakati wa kubadili mwelekeo kukomesha ubaguzi wa rangi wa kimfumo: Bachelet

28 Juni 2021

Kamishia Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet leo ametoa wito wa haraka kwa nchi kupitisha "ajenda ya mabadiliko ili kung'oa ubaguzi wa kimfumo, kama alivyochapisha ripoti ikitoa mwangaza juu ya ukiukaji wa haki za kiuchumi, kijamii, kitamaduni, kiraia na kisiasa unaowakabili  watu wa asili ya Kiafrika kila siku katika mataifa tofauti.” 

Ripoti hiyo inasema kuwa uhamasishaji wa watu duniani wanaotaka haki dhidi ya ubaguzi wa rangi umelazimisha kutambuliwa kwa suala lililochelewa kwa muda mrefu la ubaguzi wa rangi na kuhamishia mijadala kuelekea mwelekeo wa kimfumo wa ubaguzi wa rangi na taasisi zinazozifanya hivyo. 

Bi. Bachelet amesema "Hali ilivyo haiwezekani kuendelea. Ubaguzi wa kimfumo unahitaji hatua za kimfumo. Kuna haja ya kuwa na njia pana zaidi badala ya sehemu tu ya kukomesha mifumo iliyokita mizizi tangu katika karne za ubaguzi na vurugu. Tunahitaji mtazamo wa mabadiliko ambao utakabiliana na masuala yanayoingiliana ambayo yanachochea ubaguzi wa rangi na kurejea ten ana tena kwa majanga yanayoweza kuepukika ya ubaguzi kama kifo cha George Floyd. Natoa wito kwa mataifa yote kuacha kupinga kuwepo kwa unaguzi wa rangu  na badala yake waande kuutokomeza ubaguzi huo, wakomeshe ukwepaji sheria na kujenga Imani, wasikilize sauti za watu wenye asili ya Afrika na kukabili mitazamo iliyopita na kuishughulikia.” 
  

  Kuhusu ubaguzi wa rangi wa kimfumo  
  

Mwezi Juni mwaka 2020 ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) ilipewa jukumu na azimio namba 43/1 la Baraza la Haki za Binadamu kufuatia mauaji ya George Floyd nchini Marekani, kuandaa ripoti ya kina kuhusu ubaguzi wa rangi wa kimfumo ,ukiukwaji wa sheria za kimataifa za haki za binadamu  dhidi ya Waafrika na watu wenye asili ya afrika unaofanywa na vyombo vya dola, hatua za serikali dhidi ya maandamano ya amani ya kupinga ubaguzi Pamoja na uwajibikaji na kuwasaidia waathirika. 
 
Tathimini iliyofanywa na ofisi hiyo imetokana na mashauriano kwa njia ya mtandao na washiriki zaidi ya 340 wengi wao wakiwa ni wenye asili ya Afrika, zaidi ya michango 110 iliyoandikwa , ikiwemo ya matifa mbalimbali, pia tathimini ya taarifa na nyaraka zilizopo kwa umma na mashauriano zaidi na wahusika wa suala hilo. 
Kilichobainiwa na kuainishwa 
 
Ripoti hiyo inabainisha "kukosekana kwa usawa na ubaguzi wa kijamii na kiuchumi" ambao unawatesa watu wenye asili ya Kiafrika katika mataifa mengi.  

Inasema katika nchi nyingi, haswa Amerika Kaskazini na Kusini na Ulaya, watu wenye asili ya Kiafrika wanaishi kwa umaskini na wanakabiliwa na vizuizi vikubwa katika kupata haki zao za elimu, huduma za afya, ajira, nyumba za kutosha na maji safi, na pia ushiriki wa kisiasa , na haki nyingine za msingi za binadamu. 
"Kudhalilishwa kwa watu wa asili ya Kiafrika kumedumisha na kuendeleza uvumilivu kwa ubaguzi wa rangi, ukosefu wa usawa na vurugu," ripoti imeongeza. 

Katika kuchunguza vifo mikononi mwa maafisa wa utekelezaji wa sheria katika nchi tofauti na mifumo tofauti ya sheria, ripoti imegundua kwamba "kuna kufanana kwa hulka hiyo na mifumo ikiwa ni pamoja na vizuizi vinavyozikabili familia katika kupata haki. TAGS: OHCHR, HRC, Michelle Bachelet, watu wenye asili ya Kiafrika, ubaguzi wa rangi 
 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter