Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taka za plastiki zatengeneza matofali ya kujenga barabara - Gjenge Makers

Nzambi Matee, mwanzilishi wa Gjenge Makers ambayo inatengeneza matofali kutokana na taka za plastiki.
UN News/Grece Kaneiya
Nzambi Matee, mwanzilishi wa Gjenge Makers ambayo inatengeneza matofali kutokana na taka za plastiki.

Taka za plastiki zatengeneza matofali ya kujenga barabara - Gjenge Makers

Masuala ya UM

Taka za plastiki ni moja ya changamoto kubwa katika uhifadhi wa mazingira huku nchi zikifanya juhudi mbali mbali kukabiliana na changamoto hii kwani ina athari kwa viumbe na mazingira kwa ujumla.

Nchi nyingi zimepiga marufuku matumizi ya plastiki hususan mifuko hatahivyo kuna bidha nyinginezo ambazo bado zinahifdhiwa kwenye plastiki ambapo pindi tu zinapotumika bidhaa hizo plastiki hizo huishia kwenye mazingira. Kwa kutambua changamoto hiyo binti mmoja nchini Kenya ametafuta namna ya kubadilisha plastiki hizo kutoka taka hadi matofali.
Nzambi Matee anasema alianzisha kampuni ya Gjenge makers  kama wazo tu mwaka 2017 na hapo kuanza na utafiti huku akitumia mifano kutoka kwingineko ya teknolojia hiyo ambako plastiki zilikuwa zinatumiwa kutengeneza bidhaa za kujenga. 

 

Soundcloud

Gjenge makers imeanza kuuza bidhaa zake sokoni mwaka 2020 ambapo Bi Matee anasema, “changamoto ya plastiki sio ya Kenya pekee yake, taka ya plastiki ipo kila sehemu na kila nchi inatafuta namna za kukabiliana nayo na kwa kutumia masomo yangu katika sayansi nikatafiti ni mbinu ipi ninaweza tafuta suluhu kwa changamoto hii na kwa sasa tunatumia aina tatu za plastiki ikiwemo mabaki kutoka viwandani na chupa au mikebe ya plastiki inayobeba bidhaa mbalimbali."
Bi Matee anasema licha ya kwamba wazo lilikuwa la mtu mmoja sasa hivi kampuni yake imepanuka na kwa sasa inaajiri watu kumi na vibarua mara kwa mara kama inavyohitajika. Kwa sasa Gjenge inazailisha matofali 1,500 kwa siku huku akiwa na ndoto kwamba kampuni hii itakua zaidi kwani, “huu ni mwanzo tu”

Mshindi wa tuzo ya bingwa wa sayari dunia kijana

Licha ya kwamba Gjenge makers ni kampuni iliyoanzishwa miaka michahe iliyopita tayari Bi. Matee ni miongoni mwa washindi wa tuzo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP ya bingwa wa sayari dunia kijana kwa mwaka 2020. Kuhusu tuzo hiyo anasema, “kushinda tuzo inakupa motisha kwa sababu hii ni kampuni ndogo alafu pia inaweka kibali suluhisho kwa sababu hii ni suluhisho mpya kwenye soko sio kitu cha kawaida hususan katika sekta ya ujenzi na licha ya kwamba watu awali walikuwa na wasiwasi kuhusu bidhaa ya plastiki kutumika katika ujenzi tuzo imefanya watilie maanani bidhaa yetu.”