Waachieni huru waliokamatwa Hong Kong- OHCHR

7 Januari 2021

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za bindamu, OHCHR, imeelezea wasiwasi wake kufuatia kukamatwa kwa wanaharakati wa kisiasa, wasomi na waliokuwa wabunge, wajumbe wa wilaya na mawakili kwenye jimbo maalum la Hong Kong SAR na kutoa wito waachiliwe huru haraka. 

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari ya msemaji wa OHCHR Liz Throssell  hatua ya kuwakamata watu hao ni ishara ya matumizi ya sheria ya kukiuka chini ya sheria ya usalama ya kitaifa ambayo inatumika kuwashkilia watu hao na kuwanyima haki yao ya kushiriki katika siasa na maisha ya umma 

Ofisi ya haki za binadamu na wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa mara kwa mara wametoa onyo kuhusu hatia kama kukiuka mamlaka ya taasisi chini ya sharia ya kitaifa iliyopitishwa mnamo Juni 2020, haieleweki n ani pana hivyo kuwacha peno la kutumika vibaya au kutekelezwa kiholela. 

Bi. Throssel amesema kitendo cha kuwakamata watu hao cha jana ni mfululizo wa kuzuiliwa kwa watu kutokana na wao kutekeleza haki yap ya msingi ikiwemo kuandamana kwa amani Hong Kong. 

OHCHR imesisitiza haki ya kushiriki katika maswala ya imma moja kwa moja au kupitia wawakilishi ni haki ya msingi iliyo katika mkataba wa kimatiafa wa haki kuhusu maswala ya umma na siasa (ICCPR) ambayo imo ndani ya sheria za Hong Kong.  

Kwa mantiki hiyo OHCHR imetoa wito kwa mamlaka kuhakikisha wanaheshimu sheria chini ya ICCPR na kujizuilia kutokana na matumizi ya sheria ya usalama wa kitaifa kukandamiza haki na uhuru wa kujieleza na kuandamana kwa amani. 

Halikadhalika ofisi hiyo imetoa wito kwa mamlaka kuhakikisha haki ya kujieleza inazingatiwa wakati huu wa uchunguzi ikiwemo kuruhusu waandishi wa habari na mashirika ya habari kutekeleza wajibu wao kikamilifu kwa uhuru. 

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud