Chuja:

#Usafirishaji haramu

22 Novemba 2021

Karibu kusikiliza jarida leo tunajikita katika mada kwa kina kuangazia harakati za kusongesha viwanda vidogo vidogo barani Afrika hususan nchini Tanzania, kwa kuzingatia kuwa mwishoni mwa wiki ilikuwa ni siku ya viwanda barani Afrika.

Pia utapata fursa ya kusikiliza habari kwa ufupi

Sauti
11'41"
Watoto wakimizi wakionesha kuunga kwao mkono shughuli za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR za kutokomeza usafirishaji haramu huko Wad Sharige Mashariki mwa Sudan.
© UNHCR/Osama Idriss

Simulizi Yangu: Kukabili usafirishaji haramu Malawi

Maxwell Matewere, mtaalamu katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuzuia uhalifu na madawa ya kulevya, (UNODC) nchini Malawi, amekuwa akiendelea na harakati zake za kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu kwa zaidi ya miongo miwili. Leo hii anapatia mafunzo maafisa mbali mbali nchini Malawi kuzuia na kukabili uhalifu: mwaka huu pekee licha ya janga la Corona au COVID-19, ameweza kuokoa watu 300 waliokuwa wakumbwa na usafirishaji haramu sambamba na kukamata watu 31 wahusika wa uhalifu huo.
 

© UNICEF/UN045727/Pirozzi

Usafirishaji haramu na changamoto zake Afrika Mashariki

Mapema wiki hii dunia imeadhimisha siku ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu huku Umoja wa Mataifa ukiutaja kama uhalifu mkubwa unaoshuhudiwa katika kila pembe ya dunia. Vita, mabadiliko ya tabicnhi,

umasikini na ubaguzi ni baadhi ya vitu ambavyo vimetajwa kuchochea wasafirishaji haramu kutumia fursa hizo kuendeleza biashara zao za kihalifu. Umoja wa Mataifa unahimiza kwamba juhudi za pamoja ni muhimu katika kusaidia kukomesha uhalifu huo na kuwaadhibu wahusika.Je nchi zinapambana vipi na uhalifu huo? namkaribisha Grace Kaneiya kwa maelezo zaidi

Sauti
5'48"
© UNICEF/UNI91025/Noorani

Kukomesha usafirishaji haramu ni jukumu la dunia nzima:UN

Usafirishaji haramu wa binadamu ni uhalifu mbaya kabisa na unagusa kila pembe ya dunia, huku waathirika wakubwa wakiwa ni wanawake, wasichana na watoto umesema leo Umoja wa Mataifa. Arnold Kayanda na ripoti kamili. 

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uhalifu na madawa UNODC ,katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu, asilimia 72 ya waathirika wa uhalifu huu ni wanawake na wasichana huku idadi ya watoto waliothirika ikiongezeka mara mbili tangu mwaka 2004 hadi 2016.

Sauti
3'55"