Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya ICT kuleta nuru katika ukuaji wa uchumi duniani:ITU

Brodbandi ya simu.
UN
Brodbandi ya simu.

Matumizi ya ICT kuleta nuru katika ukuaji wa uchumi duniani:ITU

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Utafiti mpya uliochapishwa leo na muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU ambalo ni shirika la Umoja wa Mataifa lililojikita na masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT), umetathimini kwa kina mchango wa ICT katika uchumi wa mataifa mbalimbali.

Utafiti huo “Mchango wa kiuchumi wa kanuni za brodbandi, masuala ya kidijitali na ICT” unasema  ongezeko la matumizi ya brodband yanaleta  nuru katika ukuaji wa uchumi.

Ukigeukia mabadiliko ya kidijitali utafiti huo unaonyesha kwamba mchango wa kiuchumi wa kukumbatia mabadiliko hayo ni mkubwa, sawa na ule unaoletwa na matumizi ya brodband kupitia simu za rununu au simu za kiganjani.

Utafiti pia umebaini kwamba sera muafaka na zinazofanya kazi pamoja na mikakati bora vinaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi kupitia mfumo wa kidijitali. Na kwa mantiki hiyo Houlin Zhao katibu mkuu wa ITU amesema “kwa utafiti huu wa kihistoria sasa tunaweza kuthibitisha matokeo ya usambazaji wa broadband na mabadiliko ya kidijitali katika ukuaji wa uchumi, na kwamba uwekezaji katika miundombinu ya ICT ni kipaumbele cha kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za broadband, na pia kusaidia kuharakisha mafanikio ya Malengo ya Maendeleo Endelevu au SDG’s."

Kwa mujibu wa ITU utafiti huo pia umesema kupitia mfumo ambayo ni mifano ya kuigwa, kanuni pamoja na mpango wa kuchunguza athari za kiuchumi za broadband na kuwezesha uchambuzi kamili wa takwimu za mabadiliko ya kidigital kutasaidia kutoa ushahidi kwa kuzingatia uundwaji wa sera a maendeleo yanayopatikana.