Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN waungana na dunia kuadhimisha siku ya kimataifa ya Yoga

SIku ya kimataifa ya Yoga katika makao Makuu ya Umoja wa Maifa
UN Photo/JC McIlwaine
SIku ya kimataifa ya Yoga katika makao Makuu ya Umoja wa Maifa

UN waungana na dunia kuadhimisha siku ya kimataifa ya Yoga

Afya

Leo ni siku ya kimataifa ya Yoga ambayo inaadhimishwa na Umoja wa Mataifa kwa mwaka wa tano sasa. Mwaka huu 2019 maudhui ni “Yoga na hatua dhidi ya mabadilikoya tabianchi”

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa siku ya Yoga ambayo kwenye Umoja wa Mataifa imeanza kuadhimisha Alhamisi usiku kwa matukio mbalimbali ikiwemo darasa maalum la kufanya Yoga kutoka kwa nguli au Gulu wa Yoga ni fursa muhimu ya watu kutafakari masuala yanayoihusu duniani kama mabadiliko ya tabianchi.

Maaadhimisho haya yameandaliwa na ujumbe wa kudumu wa India kwenye Umoja wa Mataifa ukishirikisha maguru wa Yoga Swami Paramananda, Kevin Tobar na Sunaina Rekhi ukihusisha pia burudani ya muziki na dansi.

Mgeni rasmi amekuwa naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohamed ambaye pia alishiriki darasa la Yoga.

Leo kwenye Umoja wa Mataifa kunafanyika mijadala miwli kuhusu Yoga na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi tatizo ambalo Bi. Mohammed amesema “Hatua madhubuti zisipochukuliwa sasa kulikabili , atahri zake zitakwenda vizazi na vizazi.”

Mabadiliko ya tabianchi ni moja ya mtihani mkubwa unaoikabili dunia hivi sasa na Umoja wa Mataifa uko mstari wa mbele katika vita hivi ukitoa wito kwa wadau wote kuanzia serikali, sekta binafsi, asasi za kiraia na kila mtu kuchukua hatua ili kunusurua kizazi hiki na vijavyo.

Siku ya kimataifa ya Yoga huadhimishwa kila mwaka Juni 21.