Mradi wa UNHCR Kenya sio tu unasaidia wakimbizi lakini pia jamii zinazowahifadhi

18 Aprili 2019

Wakimbizi na jamii zinazowahifadhi nchini Kenya, wamepata mbinu ya kujipatia kipato huko Kolobeyei, kambi ya Kakuma  kufuatia ufadhili wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini humo na wadau wengine ikiwemo serikali ya Marekani

Mradi huo wa UNHCR na wadau unawapatia wakimbizi na wanajamii wanaowahifadhi vifaa kwa ajili ya kushona shanga ambazo zinauzwa kwenye kituo cha wageni kambini.

Regina Nanok, miongoni mwa wenyeji wanaopatia hifadhi wakimbizi, ni mmoja wa wanufaika wa mradi huu anasema, "ninashona ushanga wa wanawake. Ninakopata ushanga, ni UNHCR wanatufadhili wanatuletea  vifaa na tunatengeneza, wageni wakija tunawauzia.  Inatuchukua kama siku  mbili kutengeneza. Kwa mkufu tunauza 800 fedha ya Kenya, na kwa hereni tunauza  200."  

Bi Nanok hakuficha furaha yake kuhusu faida za mradi, "kwasababu hii kazi inanisaidia mahitaji yangu ninawalisha watoto na inasaidia kazi zangu nyingine za pembeni, ningependa kuishukuru UNHCR kutuwekea kituo hiki na pia niishukuru serikali ya Marekani kwa kuwafadhili hawa ndiyo wakatuwekea kituo hiki cha kuwasaidia wakimbizi."     

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud