Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola bilioni 1.08 zahitajika kusaidia wasomali 3.4 na misaada ya dharura

Kijana akipitia maeneo yaliyokumbwa na mafuriko katika mji wa Belet Weyne Somalia.
Picha ya UM/Ilyas Ahmed
Kijana akipitia maeneo yaliyokumbwa na mafuriko katika mji wa Belet Weyne Somalia.

Dola bilioni 1.08 zahitajika kusaidia wasomali 3.4 na misaada ya dharura

Msaada wa Kibinadamu

Mashirika ya kibinadamu na serikali ya shirikisho ya Somalia leo wamezindua ombi la dola bilioni 1.08 kwa ajili ya mpango wa misaada ya kibinadamu kwa mwaka 2019. 

Taarifa ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na serikali ya  Somalia iliyotolewa leo mjini Mogadishu imetoa wito kwa wafadhili kutoa fedha kwa ajili ya wasomali walioarithiwa na mabadiliko ya tabianchi na ufurushwaji kote nchini.

Taarifa hiyo imesema kuimarika kwa uhakika wa chakula kufuatia mvua, na uwasilishaji misaada ya kibinadamu mwaka mzima umesababisha kupungua kwa asilimia 32 watu walio na mahitaji, kutoka watu milioni 6.2 hadi watu milioni  4.2 mwaka 2019. Hatahivyo athari za mabadiliko ya tabianchi na mizozo huenda ikaathiri hatau zilizopigwa.

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Peter de Clercq amesema, “isipokuwa mashirika ya misaada ya kibinadamu yatataendeleza operesheni zake au kuziimarsiha hususan katika maeneo ambako kunashuhudiwa ukame, kuna tishio katika kupoteza mafanikio kutokana na hatua ambazo tayari zimepigwa, kwani Somalia inasalia katika moja ya mizozo ya muda mrefu duniani.”

Kwa upande wake, serikali ya Somalia imeyapongeza mashirika ya kutoa misaada kwa kipaumbele chao cha kuokoa maisha na kujengea jamii stahamala.

Halikadhalika Somalia imetoa wito kwa wahisani kusaidia katika kutatua changamoto za maendeleo nchini humo huku ikisisitiza utayrai wake kushirikiana na mashirika hayo.

Licha ya changamoto za kiusalama na ufikiaji maeneo, mashirika ya misaada ya kibinadamu yalifikia watu takriban milioni 3 kila mwezi na huduma muhimu mwaka 2018.

Ombi la mwaka huu wa 2019 linalenga mahitaji ya dharura ikiwemo ya wakimbizi wa ndani, jamii zinazowahifadhi wakimbizi na wakimbizi wanaorejea nyumbani kutoka nchi jirani ikilenga mambo manne ambayo ni: msaada wa mahitaji ya dharura, lishe, ulinzi na kujengea stahamala watu walioko hatarini.