Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia inahitaji msaada kushughulikia watu wanaoteseka.UN

Peter de Clercq(kushoto) Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu misaada ya kibinadamu ya OCHA nchini Somalia akiwa kijiji cha Habasweyne kilichokabiliwa na ukame
Picha ya UN/Ilyas Ahmed
Peter de Clercq(kushoto) Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu misaada ya kibinadamu ya OCHA nchini Somalia akiwa kijiji cha Habasweyne kilichokabiliwa na ukame

Somalia inahitaji msaada kushughulikia watu wanaoteseka.UN

Msaada wa Kibinadamu

Mkutano wa kutafuta pesa za kufadhili kushughulikia masuala ya kibinadamu yanayoikabili Somalia unafanyika mjini London nchini Uingereza.

Lengo la mkutano huo ni kutafuta dola milioni 717. Itakumbukwa kuwa mapema mwaka huu wa 2018 ulizinduliwa mpango wa msaada wa kibinadamu kwa Somalia HRP ukitaka msukumo wa dola bilioni moja unusu kuweza kuwasaiadia watu milioni 5 .4 walio katika adha ya njaa  nchini humo. Fedha zinazohitajika ni kwa ajili ya kukabiliana na ukame ambao umekuwa ukiendelea nchini Somalia  kwa muda sasa.

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu misaada ya kibinadamu OCHA nchini Somalia, Peter de Cleque anahudhuria mkutano huo na ametoa ujumbe kwa washiriki na jamii ya kimataifa

(SAUTI YA PETER DE CLEQUE)

“ hali bado ni tete kwa sababu msaada ni mdogo sana kutokana na idadi ya wanaouhitaji. Kwa upande mwingine bado hali ni mbaya kwani tuko katika msimu wa uokosefu wa mvua kwani hadi sasa mvua hazijanyesha kwa msimu wa tano sasa …”

Ameongeza kuwa idadi ya waathirika wapya imeongezeka na kufikia milioni   tangu mgogoro huu anze mapema mwaka wa 2017. Amewataka wahisani kuongeza dau lao kwani kila mwezi wanahitaji dola milioni 100 na hadi sasa wamepata dola 129 tu za kusaidia mwaka huu jambo ambalo linaweka juhudi zao njia panda.

Mwaka jana mpango huo ulipokea  asilimia 68 ya pesa zilizoombwa ambazo hazikufikia bilioni  moja na nusu zilizoihitajika. Njaa ya mwaka 2017 nchini humo iliweza kukabiliwa kutokana hatua za awali zilizofanywa na seikali,makundi ya kiraia,sekta binafsi,  makundi ya raia wa Somalia waishio nje ya nchi pamoja na wahisani.