Harakati zaendelea mashinani kuepusha mauaji ya kimbari

7 Disemba 2018

Kuelekea siku ya kimataifa ya kumbukizi ya waathirika wa mauaji ya kimbari na kuzuia  uhalifu huo tarehe 9 mwezi huu wa disemba, makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kunafanyika tukio la kukumbuka watu hao na kuhakikisha utu kwa manusura wa vitendo hivyo.

Mkutano huo unahudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, wakati huu ambapo hata mashinani kuna harakati zinaendelea kuepusha mauaji hayo kwa kuzingatia kilichotokea Rwanda mwaka 1994.

Harakati hizo ni pamoja na zile zinazofanyika nchini Uganda ambako mwandishi wetu John Kibego amezungumza na Yusufu Bunya, msemaji wa chama cha BUKITAREPA kinachotumia vyombo vya sheria kusaka haki za jamii za watu asili za Bunyoro ili kuepuka mauaji ya kimbari na kueneza chuki za kikabila magharibi mwa Uganda, ambapo Bwana Bunya anasema..

[mahojiano]

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter