Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tukishirikishwa tuna mchango katika kutatua changamoto za dunia:Kijana Ajwang

Vijana wakiwezeshwa kupata uwezo wa kutumia kompyuta katika kituo cha UN-Habitat Kigali,Rwanda.
© UN-Habitat /Julius Mwelu
Vijana wakiwezeshwa kupata uwezo wa kutumia kompyuta katika kituo cha UN-Habitat Kigali,Rwanda.

Tukishirikishwa tuna mchango katika kutatua changamoto za dunia:Kijana Ajwang

Masuala ya UM

Vijana wanaoshiriki jukwaa la Umoja wa Mataifa la muungano wa ustaarabu mjini New York Marekani wametoa wito wa ujumuishwaji wa vijana katika utafutaji wa suluhu ya changamoto zinazoikabili dunia hivi sasa ikiwemo kujihusisha katika vitendo vya uvunjivu wa Amani na itikadi kali.

Miongoni mwa washiriki wa jukwaa hilo lililowaleta pamoja vijana kutoka kote duniani, nchini wanachama na kuandaliwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya muungano wa ustaarabu , ni Jan Ajwang, kutoka shirika la Media Focus in Africa nchini Uganda linajihusisha na kuhamasisha vijana kudumisha amani  kupitia vyombo vya habari. Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa jukwaa hilo amesema vijana wengi wanahisi kama wametengwa kwa sababu“Sasa tunaona kwamba, sauti ya vijana haijawekwa sana kuhusu haya mambo  na ndio sababu wameweka mda mwingi kuongea na vijana wengi ili wajue jinsi vijana wanaangalia mambo…na hivyo tunaona kwamba inclusiveness ya sauti ya vijana sio kubwa sana kwani kuna pengo na ni lazima ijumuishwe.”

Kuhusu lengo la harakati zao amesema,“Tunasaidia jamii..tunaletea jamii platform ya kuongea. Tunajua kwamba mtu akikaa kimya atasumbuliwa na mawazo na atabaki na hizo hofu alizonazo dhidi ya kabila lingine, kuhusu serikali pamoja na vyombo vya ulinzi.”