Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi la msaafara wa misaada Nigeria

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi la msaafara wa misaada Nigeria

Mratibu wa shuguli za kibinadamu za Umoja wa Mataifa nchini Nigeria Bwana Edward Kallon amelaani vikali shambulizi la msafara wa misaada ya kibinadamu uliotokea tarehe 16 kazkazini mashariki mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hii, shambulizi  hilo lilitokea  katika mji wa Dikwa na Gamburu katika  jimbo la Borno na kusababisha vifo vya raia 4 na uharibifu mkubwa wa chakula kilichokua kinapelekwa kwa waathirika.

Bwana Edward amesema matukio ya ushambuliaji wa misaafara ya huduma za kibinadamu ni lazima ukomeshwe kwani unaathiri upatikanaji na haswa usafirishaji wa chakula kwa waathirika   wa vita na njaa ambao ni wanawake na watoto.

Ijulikane kwamba Umoja wa mataifa na washirika wake hufanya shughuli za kibinadamu kazkazini mwa Nigeria  kutoa huduma za kibinadamu kwa  zaidi ya wakimbizi wa ndani milioni 6.8 ambao wanakabiliwa na mahitaji mbalimbali yatokanao na migogoro ya kivita iliosababiswa na kundi la wanamgambo la  la BOKO HARAMU.